Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.

Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.

Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.

Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.

Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.

Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.

Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.

Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.
Bila shaka wewe utakuwa mwanae
 
Hahahahahahahaha unanipa fursa ya kuongeza afya yangu, umekasirishwa sans na hoja zangu? Hakuna jambo ninalolihofu katika tote uliyoyaeleza.

Mimi ni muungwana sana! Na sijihusishi na utapeli wa ain't yoyote. Nina amini kuwa ukithubutu kufanya yote uliyoyaainisha hapo katika komenti yako basi utaiita jamii ya wana Jf kukutambua vema kuwa wewe umeandika uwongo na udhalili mkubwa kwa mtu huyu.

Kuhusu kuhusika nae mtu huyu, ipo komenti hapo juu kaandika mwana Jf, ambaye ana mtazamo wa kina sana ambaye ameweza kusoma na kuelewa na sio kusoma na kujibu. Nakutaka some ili uelewe.
Sifa mojawapo ya tapeli huwa anatumia maneno mengi kufikisha/kuwasilisha jambo dogo.

Pia tapeli hutumia maneno mengi sana kufanya taswira yake ing'ae machoni pa mtu.

Take a break ujifanyie critical evaluation.
 
Wakongwe wa Ujiji ni Said Arobati, Saleh Ndauga, Kabeke, Kitama, Njemba, Omari Kakolwa, Sheikh Kitumba, Sheikh Khalfan, Yusuf Tosiri, Abdallah kitenge, Mussa Rehani, Abdallah Chakuwa, Ganja Smoking, Saadan Abdul Kandoro, Snow White, Mohammed Saddallah, King Seleman, Issa Maganya, Mzee Mnukwa, Abubakar Mwilima, Jumapili Kasongo, Mzee Kocho, Issa Sadiki, Mzee Saliboko, Nk
Hujamtaja Abdallah Said,
 
Hakufa wapo wawili sio mkoba Bali elimu ya kitabu na kuburi tu. Hats wachungaji wapo wenye nguvu na uwezo wa Mungu katika kuitikiwa maombi
Mkuu hyo ELIMU YA KITABU unayozungumzia ndio uchawi wenyewe,uchawi sio lazima kutumia tunguli na kaniki,nyie ndo mnapotosha watu wanaenda kwa hao wanaojiita 'mashehe' wanaandikiwa makombe na zafarani,kupewa mipete wakidhani ni halali mwisho wake uislamu unapakwa matope.Narudia tena yale aliyokuwa anafanya marehemu shehe yahya and the likes ni uchawi/ushirikina.Hayo mavitabu ni manuals tu.na kwa vile mengi wanayoyatumia yanalugha ya kiarabu ndo kabisaa watu wanaingia mkenge.
 
Nami nitoe mtazamo wangu kuhusu Likud na AbuFizzer

Kwanza niseme tu Mimi ni mzaliwa wa Gungu(kigoma), japokuwa umri wangu ni late 20s kuna mambo machache nayafahamu kuhusu Juma Njemba.

Mvutano kati ya Likud na Abufizzer ni wa kutaka kuonesha kuwa nani anamfahamu Zaidi Juma Njemba. Likudi ameelezea dark side ya mzee huyu maarufu wa kimanyema ambapo katika Maelezo yake, kuna ukweli mwingi na mengine ni chumvi. Mfano, hilo la kuoa wake 200 Nina shaka nalo,

Abufizzer anaonekana kuwa ndugu wa karibu wa Njemba au moja ya wana familia wa ndani. Anachofanya kutetea kuwa mzee Njemba hakuwa anaogopeka kwa mambo hayo ni kutaka kutunza siri ya familia tu. Mara nyingi watu wanaofanya shughuli hizi za kichawi na kishirikina huwa wanajificha kwenye dini ya kiislamu na kujifanya wasomaji wa kitabu cha quraan. Ila kiukweli, wanaua, wanatibu, wanafanya kila aina ya mandava ya darkside.

Mengi aliyosema LIKUD ni kweli, na anayosema Abufizzer ni "story counterbalance" tu.

Njemba aliogopeka, achana na yule jamaa
 
LIKUD nakushukuru kuknikumbusha story ya mzee wangu wa ujiji huyu mzee kwa wafanyabiashara wa mikoa ya Tabora, Mwanza, Kigoma, Shinyanga na wale wa nchi kama Rwanda na Burundi ikiwamo Congo watakumbuka zindiko lake la kupita na magendo bila kuonwa wala kukamatwa na askari na dawa ile ilikua mnapita mnaondoka askari mnawaona wao hawawaoni hata iwe mchana.
kuna watu eti wanabisha humu"" huyo juma njemba alikuwapo kweli " wazazi wangu waliwahi nihadithia habari zake " aiseee alikuwa nimtu hatari mnooo", though ninarafiki yangu aliwahi kumuoa mjukuu wake but now wameshatalikiana " na " huyo rafiki yangu anaishi UAE kwa sasa
 
Anajuaje kama ataenda mbinguni au peponi??? But anyway jamaa alifanya mambo mengi sana yasiyompendeza Mungu kwa kweli.........

Na jamaa naskia kweny kazi yake alikua hapokei hela yako mpka uone matokeo....sasa ww akufanikishie mchongo afu usimlipe....weeeeeeeee anasomba nusu ya ukoo wako
hahaaaa ati nusu ya ukoo wako
 
Tupe na za yule Mzee wa kagunga aliekuwa ikifika usiku anatandika mkeka juu ya ziwa Tanganyika anakwenda kulala Burundi.
acha masiharA basii mkeka juu ya maji ""?
 
Hilo zindiko ni hatari sana linahitaji ujasiri wa hali ya juu..Alikuwaga pia na zindiko la kumzika MTU kaburini, MTU kupikwa kwenye pipa pamoja na Yale ya " kusafiri" kwenda kuzimu kama lile lililo muua Joseph Kabasele
mmmh mkuu huyo kabasele alifanyaje hebu tupe dodosa kidogo""
 
Back
Top Bottom