Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Uliyesema amerithi kazi Njemba anafanya kazi zipi sasa kama bado mnasema "Njemba angekuwepo.....!!!?"
Hakuna aliyerithi mkuu aliye rithi alisha kufa toka enzi za Pontyo wa Pilato..Usikubali kudanganywa na kulaghaiwa
 
Huyo AbuFizzer anataka kulaghai watu mkuu... Juma Njemba hana mrithi YOYOTE wa kazi zake...Be warned in advance
Mkuu kwenye jina nimemuuliza mtu akaniambia ni inrahim ila swala la juma njemna nalilijua na kwa kigoma hiyo chamtoto ushaisikia ya mtu aliekufa kwa mujibu wa hospitali na motwari aliwekwa 2 days lakini ni mzima hadi leo
 
Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.

Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.

Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.

Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.

Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.

Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.

Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.

Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.
Duhhh watu hatari Sana'a..
Sasa anawezaje kuwasumbua wachawi kma yeye sio mchawi piaaa,..mwenye nguvu kubwa
 
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.

Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.

Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.

Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.

Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.

Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka

Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.

Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.

KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."

Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.

Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..

MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.

Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.

Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.

"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "

" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.

Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.

Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.

Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..

Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.

Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua


Hii siamini, ngoja niwaulize Waha mashuhuri wa Ujiji kina Diamond na Zitto.
 
Ndio Zitto anatishia nyau watu wanaowachezea watu wa Kigoma kwa kutumia historia ya huyu nini?
Kaka niamini mm watu wa kigoma sio mchezo niliishi kule 2 yrs nilijionea makubwa nikiwasimuli watu huwa hawaamini mfano kigoma kuna mganga anaweka kinga ya sumu akimaliza kitest unakunywa sumu ya panya uliyonunua mwenyewe ,kwa macho yangu alienisimulia alisaga vioo na kumeza na bia
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu usitake nifunguke mazito kama kabwe
Huna ujualo, Huna utakachofunguka, mzee Yule alikuwa an mwanafunzi wake aliyeishi nae an kumpa ufundi kwa miaka 34, humjui

Mzee Yule ana mwanafunzi wake yupo Dodoma eneo linaitwa Majengo humjui

Mzee Yule alikuwa na marafiki zake kina Sebastian Kinyondo, Gama, Mussa Kwikima

Wakuu wa mikoa waliridhika kumwita baba, viongozi wa nchi walimtembelea kwa uficho. Huna unalojua.
 
Kaka niamini mm watu wa kigoma sio mchezo niliishi kule 2 yrs nilijionea makubwa nikiwasimuli watu huwa hawaamini mfano kigoma kuna mganga anaweka kinga ya sumu akimaliza kitest unakunywa sumu ya panya uliyonunua mwenyewe ,kwa macho yangu alienisimulia alisaga vioo na kumeza na bia
Hatishii Zitto ni mzima, wazee wote walimridhia wakiwemo watoto wa huyu mzee
 
Back
Top Bottom