Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
Tueleze mkuu
 
Kwan kati ya juma njemba Na bint Rukungu nani alikua mchawi mkubwa kumshinda mwenzie? Hizi story ulisimuliwa na wewe umekuja kusimulia Kweli huyo mtu alikuepo huko ujiji lakin umeongeza chumvi nyingi
 
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.

Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.

Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.

Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.

Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.

Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka

Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.

Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.

KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."

Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.

Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..

MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.

Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.

Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.

"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "

" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.

Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.

Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.

Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..

Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.

Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Uongo huu
 
siaminigi uchawi hatakidogoo

We bwana, sema hivi:- "namuomba Mungu anilinde na wachawi", na wala usiseme kuwa huamini uchawi kwani uchawi ni elimu au dhana pana mno na kimsingi ni ile inayoitwa (hypnotism /mesmerism) ambapo mtu mwenye hiyo elimu anapoitumia vibaya ndipo inapoleta madhara kwa watu na mara nyingi inatokea watu wenye elimu hiyo hujiona wamepata nguvu na huanza kujiamini na kusahau kuwa yupo mwenye nguvu zaidi yao yaani Mungu na ikifika hatua hiyo ndipo huyo mtu huitwa mshirikina basi hapo ushetani unaingia na maramoja mtu huyo anakuwa ni hatari sana kwa watu kwani anakosa hofu juu ya Mungu.
 
LIKUD nakushukuru kuknikumbusha story ya mzee wangu wa ujiji huyu mzee kwa wafanyabiashara wa mikoa ya Tabora, Mwanza, Kigoma, Shinyanga na wale wa nchi kama Rwanda na Burundi ikiwamo Congo watakumbuka zindiko lake la kupita na magendo bila kuonwa wala kukamatwa na askari na dawa ile ilikua mnapita mnaondoka askari mnawaona wao hawawaoni hata iwe mchana.
Mmhh kweli???
Duh
 
Kwan kati ya juma njemba Na bint Rukungu nani alikua mchawi mkubwa kumshinda mwenzie? Hizi story ulisimuliwa na wewe umekuja kusimulia Kweli huyo mtu alikuepo huko ujiji lakin umeongeza chumvi nyingi
Alikuwepo Leo nilikua na dogo mmoja wa kigoma huko maarufu ukoo wao nikamuulizia eti wamjua Juma Njemba akasema 'weee acha Dada angu alikua gwiji la uchawi huyo anaoa na kuacha na bamdogo ndo alikua mshenga wake yaani akila jiwe dogo kwenye wali talaka'

Yaani aliyoyasema Likud yana ukweli 96% yaani hao watetezi wake ni wasanii tu wanamsafisha mushriki kama huyo mchawi ...

Alikua anasemaje "sawa mi ntachomwa moto kesho kwa Mungu lakini na Mimi hapa duniani nkikutaka sikuachi"
 
mimi niluwahi kwenda kwa huyo mzee lakini niliogopa kumalizia zindiko la milango saba ya ziwa tanganyika, nikaondoka kwa kutoroka tukiwa mlango wa tatu , nadhani umenikumbusha mbali mno wala hujakosea kitu.
Ayo mazindiko ya milango yakoje?
Tuellezee japo milango mitatu tuu
 
Wacha urongo..Juma Njemba alifariki mwaka 2001 na alikufa kwa kiharusi cha kisheitwani...Chanzo cha kifo chake ni kuzidiana nguvu kati ya uchawi wake na kinga ya MTU ambae Juma Njemba alitaka kumuua kwa uchawi.

Kombora alilo piga Juma Njemba kwenda kumuua MTU huyo liligonga mwamba na kumrudia yeye mwenyewe na siku kadhaa baadae alifariki dunia...Unataka nifunguke zaidi what happened ?

Juma Njemba alipigwa Back To Sender
Umenifanya nicheke saana mkuu.. BACK TO SENDER. [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Shetani ni Mungu pia.. Anyways usitutoe kwenye Uzi..Nina nondo nyingi sana kuhusu huyu jamaa aitwae Juma Njemba ...Vituko na matukio yote makubwa aliyo yafanya..Ntashindwa kutiririka vizuri kwa sababu ya tapeli mmoja anae taka Ku capitalise kwenye hiyo fact ili awalize watu..please boy cot him
6

"Shetani ni Mungu pia---?!!!," Vipi kauli hii mbona imekaa vibaya mno 😫, Hebu nakuomba uitengue kabla Mungu hajashusha hasira zake kwa kumfanisha na hilo dubwashika.
 
Wajibu wako kama member wa familia yake kikweli umeutekeleza vyema sana, na popote alipo anaona hilo kwa namna ulivyo jitahdi kumtetea! Hata mimi ningefanya kama wewe, katika kumtetea mzazi wangu japo umeshindwa kijificha wewe ni nani wake, ningefanya same as you!

Hapo juu ya comment yako, yupo member mwingne amakuja kutoa ushuhuda kuwa, kipindi kinatangazwa kifo cha huyu mzee, misikiti mingi au karibu yote huko watu walishangilia.....kauli inayo endana na mtoa mada!
Baadhi ya maswali ulioshindwa kutufafanulia, ni kuwa inakuwaje malaika au mtakatifu wa aina yake akaogopwa kiasi hicho? Kwanini watu walishangilia? Kuna anaye shangilia kifo cha mtu aliye mwema na alie msaada kwa jamii au the opposite?

Kabla hujamaliza, ningependa uiandike tena tarehe yake aliokufa ili ikae kwnye rekodi humu mkuu!
Walioshangilia kifo chake ni watu waovu waliokuwa wanashughulikiwa na Njemba......Mwaka 2002 wakati nachimba madini ya dhahabu Kigoma Karenge wachimbaji wengi sana walisaidiwa na Njemba....Wachawi wote walikuwa wanamuogopa sana Njemba
 
Back
Top Bottom