Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Nimesikiliza BBC leo jioni na kumsikiliza huyu mheshimiwa sana Juma Nkamia.
Mada yake isiyo na mbele wala nyuma ni kuongeza muda wa urais toka miaka mitano hadi saba.

Hapo ndio mwisho wake wa kufikiri!

Nimemsikiliza ndugu mmoja aliye mfundisha kuwa mantiki ya utawala ni uendelevu wa taasisi za dola, ili zifanyekazi zinazopaswa.

Jamaa wala hakuelewa.
Kwa hili hata elimu ya msingi hadi chuo kikuu nafikiri inampiga chenga.
Maana somo la DS nafikiri halimo kichwani.

Kuna mtu akatuma ujumbe kuwa huyo J Nkamia katumwa, Juma akaanza kutusi kuwa hayo ni maneno ya chumbani.

Jamani nijulisheni ,huyu Nkamia mbona ana IQ ndogo hivi?
Na anawawakilisha jimbo gani?
 
Mkamia ni kama amerukwa na akili tu. Labda hakutegemea siku moja kuja kuwapangisha UN ile nyumba yake ya pale Dodoma.
Hivyo yote ayafanyayo ni katika hali ya kupigwa butwaa tu...au akiamini analipa fadhila
 
Leo jioni kwenye dira ya dunia, Mbunge Mh. Juma Nkamia ambaye ndio muanzilishi wa mjadala wa miaka ya ukomo wa mhula wa rais kuwa 7, ametoa majibu ya hovyo kabisa kwenye mahojiano ya dira ya dunia BBC.. Wenzake wa Kenya na Uganda walikuwa wamejipanga kwa hoja ambayo hata haihusu mustakabali wa mataifa yao, lakini yeye ameshiriki ule mjadala kwa kutoa utetezi wa hoja yake with very shallow responses.
Yaani leo ndio Mtanzania wa kawaida kabisa utaamini kweli sisi tuko nyuma ya wenzetu wa Kenya na Wa UG kwa upeo wa mambo. Ilifika hatua anahoji eti kwani Chancellor wa ujerumani yuko madarakan miaka mingapi sasa? Kwani chancellor yuko pale kwa kubadilisha vifungu vya katiba au ni katiba aliyoikuta ndio inamruhusu kubakia madarakani mpaka sasa? Mimi ni CCM lakini its about time tuhandle hizi type za kina Nkamia kwa umakini mkubwa sana. Kwa mjadala wa leo pale inaonyesha dhahiri huyu jamaa amepandikizwa hii ajenda, na ndio maana amechemka kutoa majibu ya hoja nyingi pale kama wenzake wa Kenya na Uganda.
We sio CCM ndio maana umeshindwa kuwasilisha hoja.
 
Yaani amekera kinoma aisee, katufanya wote tuonekane mazuzu wa siasa... Japo Radio Free africa walijaribu kukata kata yale matangazo, bado utumbo wake alioutoa uliendelea kuskia
 
Jana nilimsikia polepole channel ten akisema kwamba swala la kuongeza muda halijawahi kuwa ajenda ya chama..

Pili alisema hayo ni mambo ya umimi, na ubinafsi mtupu..

Chama Cha Mapinduzi inamaana hawamuoni huyu Nkamia? Waache unafiki na kucheza na akili za watu.

Polepole na kundi lake waache maigizo, tuna akili!
 
Nimesikiliza BBC leo jioni na kumsikiliza huyu mheshimiwa sana Juma Nkamia.
Mada yake isiyo na mbele wala nyuma ni kuongeza muda wa urais toka miaka mitano hadi saba.

Hapo ndio mwisho wake wa kufikiri!

Nimemsikiliza ndugu mmoja aliye mfundisha kuwa mantiki ya utawala ni uendelevu wa taasisi za dola, ili zifanyekazi zinazopaswa.

Jamaa wala hakuelewa.
Kwa hili hata elimu ya msingi hadi chuo kikuu nafikiri inampiga chenga.
Maana somo la DS nafikiri halimo kichwani.

Kuna mtu akatuma ujumbe kuwa huyo J Nkamia katumwa, Juma akaanza kutusi kuwa hayo ni maneno ya chumbani.

Jamani nijulisheni ,huyu Nkamia mbona ana IQ ndogo hivi?
Na anawawakilisha jimbo gani?
Nkamia na musiba wameamua kuyakana wanayoyaamini na kuyatetea wasiyoyamini,, hivyo sioni sababu wala haja yakuendelea kuwajadili.
 
Back
Top Bottom