Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,602
- 7,344
Wakamatwe kwa kosa gani? Wao wanataka muhula uwe miaka 7, raisi amesema hataki,lakini hakuna aliyevunja sheria hata kama mmoja anasema yeye na wananchi. Kati ya mawazo yao na kutendeka kwa hicho kitu kuna kutengeneza muswada, kuna maamuzi ya bunge na kama mawazo yao yatakubalika bungeni kuna raisi (akubali au akatae) na katiba ibadilishwe. Hivyo acheni lijadiliwe na watu wawe na uhuru wao kikatiba kuunga mkono au kukataa (pamoja na maandamano ikibidi). Chama chao kinaweza pia kuchukua hatua za kichama kikiona inafaa. Lakini kikatiba kuwa na mawazo tofauti na raisi si kosa.