Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Nimesikiliza BBC leo jioni na kumsikiliza huyu mheshimiwa sana Juma Nkamia.
Mada yake isiyo na mbele wala nyuma ni kuongeza muda wa urais toka miaka mitano hadi saba.

Hapo ndio mwisho wake wa kufikiri!

Nimemsikiliza ndugu mmoja aliye mfundisha kuwa mantiki ya utawala ni uendelevu wa taasisi za dola, ili zifanyekazi zinazopaswa.

Jamaa wala hakuelewa.
Kwa hili hata elimu ya msingi hadi chuo kikuu nafikiri inampiga chenga.
Maana somo la DS nafikiri halimo kichwani.

Kuna mtu akatuma ujumbe kuwa huyo J Nkamia katumwa, Juma akaanza kutusi kuwa hayo ni maneno ya chumbani.

Jamani nijulisheni ,huyu Nkamia mbona ana IQ ndogo hivi?
Na anawawakilisha jimbo gani?
 
Hawa majamaa wamekuwa mapunga wa siasa, na wamekuwa kama vidada vya uswahilini vinacheza kila mdundiko unaokatiza mitaani kwao, yaani ni shida aisee
 
Mkamia ni kama amerukwa na akili tu. Labda hakutegemea siku moja kuja kuwapangisha UN ile nyumba yake ya pale Dodoma.
Hivyo yote ayafanyayo ni katika hali ya kupigwa butwaa tu...au akiamini analipa fadhila
 
We sio CCM ndio maana umeshindwa kuwasilisha hoja.
 
Yaani amekera kinoma aisee, katufanya wote tuonekane mazuzu wa siasa... Japo Radio Free africa walijaribu kukata kata yale matangazo, bado utumbo wake alioutoa uliendelea kuskia
 
Jana nilimsikia polepole channel ten akisema kwamba swala la kuongeza muda halijawahi kuwa ajenda ya chama..

Pili alisema hayo ni mambo ya umimi, na ubinafsi mtupu..

Chama Cha Mapinduzi inamaana hawamuoni huyu Nkamia? Waache unafiki na kucheza na akili za watu.

Polepole na kundi lake waache maigizo, tuna akili!
 
Nkamia na musiba wameamua kuyakana wanayoyaamini na kuyatetea wasiyoyamini,, hivyo sioni sababu wala haja yakuendelea kuwajadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…