Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Mnafiki mkubwa huyo,mchumia tumbo na hafai hata kua baba,hana msimamo kisa njaa.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

View attachment 2216559

Anaweza akadhani anamuumbua JPM, kumbe ndiyo anaanika ujuha wake.
Maana huko kuzuia muswada anakokusema, najua fika hakufanikiwa.
 
Vzr kajitanabaisha kua yy ni baba wa selfish wote[emoji848]
 
Nina uhakika Nkamia ni shuhuda jinsi gani watu wanajipendekeza na waoga maana baada ya hoja yake wakatokea watu kibao kumuunga mkono kumbe mwenzao alianzisha hiyo mada kunusuru ugali.

Watu wakaogopa ipinga hii hoja
 
Kumbe huyu ni kihiyo mno kiasi cha kuuanika umaamuma wake badala ya kuuficha!
 
Huyu Juma Nkamia ni kati ya wanasiasa wachovu wanaochezea mustakabali wa siasa na maslahi ya umma kwa matatizo binafsi
Angalau umesema ukweli. Huyu ndiye alikuwa mbele kabisa kusema Magufuli aongezewe muda. Ifike mahali vyama vyote vya siasa kwa umoja wao wafukuzie watu wa aina hii mbali na wasipewe nafasi yoyote. Yes, CCM wangekuwa wana akili wangemtia sasa hivi kwa unafiki wa kiwango cha juu anao uonyesha. Hata yakitokea tena mabadiliko mtu kama huyu atamnanga mama Samia.
 
Back
Top Bottom