Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

Pia soma
Jiwe bwana 😆😆,waliomjulia walitamba na kuneemeka kwa kupiga ila waliotaka kutumia akili walipata tabu Sana.

Ogopa Sana mpumbavu/ kichaa akishika rungu 😁😁
 
Kwa hiyo alitaka katiba ya nchi ivunjwe ilimradi watoto wake waende shule sio, hakuna mtu hapo.
 
CCM wengi wanafiki wakubwa including Rais Samia, na CCM wenzie wameshamwona yeye ndiye mnafiki namba moja. Haiwezekani serikali ambayo yeye alikuwa namba 2 leo eti anainanga, naweza kusema ni zaidi ya unafiki. Tusimshangae Nkamia, hiyo tabia ni jadi yao.
 
Kuna mtu wa kumnyooshea Nkamia mkono humu? Mbona sisi tumejificha na fake ID? Mbona mmekubali kuongozwa na Samia na Majaliwa ambaye wamekiri hadharani na kwa vitendo hawakuwa na Magufuli? Wako wapi watanzania waliodhubutu kusema kweli kipindi hicho, zaidi ya Lissu,Lema, Mbowe na wengine wachache ambao waliishia kutaka kuuliwa na kubambikizwa kesi

Hao viongozi wenu wa dini ndio walikuwa mstari wa mbele kwa unafiki,sembuse Nkamia?
 
Wajameni si waendage tu kulala nyumbani kwao
1652004794843.png
 
Jiwe bwana 😆😆,waliomjulia walitamba na kuneemeka kwa kupiga ila waliotaka kutumia akili walipata tabu Sana.

Ogopa Sana mpumbavu/ kichaa akishika rungu 😁😁
Wewe ni chawa wa Samia,kama Magufuri alipenda sifa huyo Mkamia na Kessi wa mkasi, mbona wote walipigwa chini kwenye kira za maoni? Magufuri alikuwa Mtu wa kazi,wazembe na wavivu ndio walimtungia uongo Magufuri
 
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

Pia soma
Jiwe alikuwa Katiri sana !
 
Wewe ni chawa wa Samia,kama Magufuri alipenda sifa huyo Mkamia na Kessi wa mkasi, mbona wote walipigwa chini kwenye kira za maoni? Magufuri alikuwa Mtu wa kazi,wazembe na wavivu ndio walimtungia uongo Magufuri
Walipigwa chini na WAJUMBE wa Magufuli waliojaa maelekezo.
 
Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa tena na wananchi. Maana ni muoga, hajiamini, mbinafsi, mnafiki na mchumia tumbo.
Wabunge wa Ccm hawahitaji uaminifu wako,akishapitishwa na Chama imeisha hiyo
 
Back
Top Bottom