Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Dah!! This is not good! Hata kama...aisee
 
Itakuja Kutokea Kwa Hangaya Pia. Ts a matter of Time Mzee Wangu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hata huyu Nkamia anavyofanya hivi ni kwa kuwa anaona upepo umebadilika.

Wale walionaswa wakimteta JPM kina Kinana na Nape wamerudishwa.

Kashasema watoto wanasoma anawatafutia ugali.
 
Sasa wa hovyo kivipi? Mtu anasomesha watoto wewe ulikua unatakaje kwani kumsifia jiwe ilikuwa inahitaji sh.ngapi ili ku survive?
Ndiyo anafanya yote hayo.
Lakini ni hulk ya ovyo sana kwa mtu kuwa nayo!
 
Kwa hiyo Nkamia anataka tuseme kuwa yeye ni mwerevu na JPM alikuwa mpumbavu?

Nchi hii ina wanasiasa wa hovyo sana
 
Hizo ndiyo siasa zetu. Kuzungumza hata bila kufikiria. Okay sasa hii inasaidia nini? Au kufukuzwa kwa Nkamia kuna impact gani kwa nchi. Anajiosha tu alijaribu kujipendekeza kwa hoja ya miaka 7 akiwa amelenga uteuzi.
 
Kuna mtu wa kumnyooshea Nkamia mkono humu? Mbona sisi tumejificha na fake ID? Mbona mmekubali kuongozwa na Samia na Majaliwa ambaye wamekiri hadharani na kwa vitendo hawakuwa na Magufuli? Wako wapi watanzania waliodhubutu kusema kweli kipindi hicho, zaidi ya Lissu,Lema, Mbowe na wengine wachache ambao waliishia kutaka kuuliwa na kubambikizwa kesi

Hao viongozi wenu wa dini ndio walikuwa mstari wa mbele kwa unafiki,sembuse Nkamia?
Ukweli mchungu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mie nafikiri kuna haja ya kumpongeza mkamia, kwani alifanikiwa kujitetea kwa kwa mbinu hiyo, je, wanaomshutumu mkamia hajui alikuwa anapambana na mtu wa namna gani, tuombe Mungu asipatikane mtawala kama bwana yule, ili akuelewe lazima ujidhalilishe, ndio utakuwa salama!
 
Hiyo ndiyo taswira ya wabunge wAliowengi wa CCM ,huwa misimamo yao inafuata upepo unakoelekea,tangu wamepitisha tozo kwenye miamala nawaona mabogus kabisa,wapo bungeni kwa maslahi yao binafsi,si ya wananchi wanaowawakilisha.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

Pia soma
Asante Hayati JPM Magufuli (R.I.P), sasa tunawajua watanzania ambao hawatufai kutuwakilisha na wale ambao wanatufaa kutuwakilisha.
 
Back
Top Bottom