Jumaa Aweso amehitisha ratiba ya ziara ya kikazi ya kimkakati nchini China kwa kutembelea viwanda mbalimbali vya kutengeneza na kuzalisha Mita za Maji

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
AWESO ATEMBELEA VIWANDA VYA KUZALISHA MITA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA CHINA, ASEMA WAKATI WA MABADILIKO NI SASA

Shangai, China

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehitisha ratiba ya ziara ya kikazi ya kimkakati nchini China kwa kutembelea viwanda mbalimbali vya kutengeneza na kuzalisha Mita za Maji za Malipo (PRE-PAID WATER METERS) kabla ili kujionea teknolojia mbalimbali katika kutengeneza mita hizo.

Waziri Aweso ameambatana na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Mwajuma Waziri, Kitengo cha Manunuzi, Idara ya Usamabaziji maji na usafi wa Mazingira, Kitengo cha Sera na Mipango, Mhandisi wa Maji, Mkaguzi wa ndani, na wataalamu wengine.

Akifafanua mkakati wa Wizara ya Maji Waziri Aweso amesema Timu hii baada ya kujionea uzalishaji na aina mbalimbali ya Mita hizi , itaungana na Kamati maalum aliounda Wizarani na kwa pamoja zitakuja na muongozo wa namna gani utekelezaji wa mabadiliko haya utakavyofanyika hatua kwa hatua.

Aidha, Aweso akiwa katika ziara hii amesema ni wakati sahihi wa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuelekea kwenye mabadiliko ya Mita za Maji kutoka zile za kawaida na kuanza kutumia mita za kisasa za Malipo kabla na kusisitiza kwamba wakati wa mabadiliko ni sasa.

Akihitimisha ziara yake viwandani Ningbo na Dhangai China, Mhe Aweso amesema pamoja na uhitaji wa mageuzi haya lakini upo umuhimu wa kujiridhisha na kufanya utafiti wa kutosha juu ya mita sahihi kwaajili ya matumizi ya nchi yetu zitakazozingatia ubora, uzalishaji toshelevu, uendelevu na thamani ya fedha ili zisiwe changamoto kwa wananchi.
IMG-20240625-WA0006.jpg
IMG-20240625-WA0007.jpg
IMG-20240625-WA0008.jpg
IMG-20240625-WA0009.jpg
IMG-20240625-WA0010.jpg
IMG-20240625-WA0011.jpg
 
Aseme tu yeye na hiyo timu yake wameenda kutalii. Hakuna jipya litakalo patikana kwenye hiyo ziara. Kama ni kero ya upatikanaji wa maji safi na salama, bado itabakia palepale.
 
Aboreshe kwanza upatikanaji wa maji maji hakuna sababu hamna DAWASA hii kweli miezi mitano inaripoti na hakuna majibu?
 
Ni hatua nzuri, japo madudu yatakayofanyika hapo kuoata mzabuni mungu anajua.

Waboreshe na upatikanaji wa maji sasa.
 
AWESO ATEMBELEA VIWANDA VYA KUZALISHA MITA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA CHINA, ASEMA WAKATI WA MABADILIKO NI SASA

Shangai, China

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehitisha ratiba ya ziara ya kikazi ya kimkakati nchini China kwa kutembelea viwanda mbalimbali vya kutengeneza na kuzalisha Mita za Maji za Malipo (PRE-PAID WATER METERS) kabla ili kujionea teknolojia mbalimbali katika kutengeneza mita hizo.

Waziri Aweso ameambatana na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Mwajuma Waziri, Kitengo cha Manunuzi, Idara ya Usamabaziji maji na usafi wa Mazingira, Kitengo cha Sera na Mipango, Mhandisi wa Maji, Mkaguzi wa ndani, na wataalamu wengine.

Akifafanua mkakati wa Wizara ya Maji Waziri Aweso amesema Timu hii baada ya kujionea uzalishaji na aina mbalimbali ya Mita hizi , itaungana na Kamati maalum aliounda Wizarani na kwa pamoja zitakuja na muongozo wa namna gani utekelezaji wa mabadiliko haya utakavyofanyika hatua kwa hatua.

Aidha, Aweso akiwa katika ziara hii amesema ni wakati sahihi wa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuelekea kwenye mabadiliko ya Mita za Maji kutoka zile za kawaida na kuanza kutumia mita za kisasa za Malipo kabla na kusisitiza kwamba wakati wa mabadiliko ni sasa.

Akihitimisha ziara yake viwandani Ningbo na Dhangai China, Mhe Aweso amesema pamoja na uhitaji wa mageuzi haya lakini upo umuhimu wa kujiridhisha na kufanya utafiti wa kutosha juu ya mita sahihi kwaajili ya matumizi ya nchi yetu zitakazozingatia ubora, uzalishaji toshelevu, uendelevu na thamani ya fedha ili zisiwe changamoto kwa wananchi.
View attachment 3025492View attachment 3025493View attachment 3025494View attachment 3025495View attachment 3025496View attachment 3025497
Kumbe mwamba hayupo,ndio maana wakazi wa Dar wanalia maji hakuna...
 
Back
Top Bottom