Pre GE2025 Jumaa Aweso inadaiwa ndio anayepigiwa Chapuo kuwa Waziri Mkuu 2025-2030 kama CCM itashinda

Pre GE2025 Jumaa Aweso inadaiwa ndio anayepigiwa Chapuo kuwa Waziri Mkuu 2025-2030 kama CCM itashinda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wetu Dokta Samia Suluhu Hassan, inadaiwa anataka kuchanganya damu changa sababu kazungukwa na wazee wakina Wasira na Mizrengo Pinda.
View attachment 3217686
Jumaa Aweso ameonekana ni Mchapakazi, sio mla Rushwa wala hana Biashara katika Soko la Kariakoo. Hivyo hawezi kuhujumu Uchumi kwa cheo chake

Hivyo inadaiwa eti ndo chaguo namba moja la Mama wa Kizimkazi(Mamalao)
View attachment 3217685
Je, nini maoni yako juu ya Uteuzi huu?

Kwa wale wasiomjua, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) alizaliwa tarehe 22 Machi 1985, Pangani, Mkoani Tanga. Mheshimiwa Aweso alisoma katika Shule ya Msingi ya Mwambao, Pangani, Mkoani Tanga (1994-2000) na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Bagamoyo (2001-2004). Mhe. Aweso alipata Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Pugu (2005-2007).
View attachment 3217684
Kati ya mwaka 2007 na 2009, Mheshimiwa Aweso alihudhuria Chuo cha Ualimu cha Morogoro na kutunukiwa Astashahada ya Ualimu. Mheshimiwa Aweso ana Shahada ya Sayansi katika Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa mwaka 2013. Mwaka 2018-2020 Mheshimiwa Aweso alihudhuria na kuhitimu Shahada ya Pili ya Utawala na Uongozi (Governance and Leadership (MAGL) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
View attachment 3217687
Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Pangani lililopo Mkoani Tanga mwaka 2015. Mwezi Oktoba 2017, Mhe. Aweso aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akichukua nafasi ya Mhe. Kamwelwe aliyeteuliwa kuwa Waziri.
View attachment 3217688
Oktoba 2020, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso alipita bila kupingwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Pangani kwa Awamu ya Pili, 2020-2025. Mwezi Desemba 2020, aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji.
View attachment 3217689View attachment 3217690View attachment 3217691View attachment 3217692View attachment 3217693
Hussein Mohammed Bashe (MB)
 
Kwa Tanzania lolote linawezekana. Kwa aina ya viongozi tulionao nchi hii, mtu yeyote anaweza kushika nafasi yeyote. Kila la heri kwake
 
Back
Top Bottom