JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo katika Kata ya Kunduchi katika mtaa wa Tegeta, jijini Dar es Salaam Mhe. Aweso amesema lengo la kampeni hii ni kuhakikisha wananchi wanasikilizwa changamoto walizonazo za upatikanaji wa huduma ya majisafi na kutatuliwa kikamilifu.
Ameiagiza DAWASA kutekeleza zoezi hili kwa ufanisi na kuelekeza nguvu kwenye maeneo ya wateja ambayo hayana huduma ya maji na sio tu kwa wateja wenye maji.
"Watu wasiteseke kupata huduma ya maji na pale panapokuwa na ulazima wa kusitisha huduma kwa muda, wateja wapewe taarifa mapema ili waweke akiba ya maji mapema," ameeleza Mhe Aweso.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa Mamlaka imepokea maelekezo ya Serikali na imejipanga vyema kupokea na kutatua changamoto walizonazo wananchi za huduma ya maji.
Ameongeza kuwa katika kampeni hii ya DAWASA mtaa kwa mtaa, Mamlaka itaenda kuhakikisha inafuatilia kwa ukaribu kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi, kuhakikisha wananchi wanaufahamu juu ya usomaji wa mita za maji.
Naye Diwani Kata ya Kunduchi, Michael Urio ameitaka DAWASA kuongeza mawasiliano na Taasisi nyingine ikiwemo Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) hususani wakati wa utekelezaji wa miradi kwa lengo la kunusuru uharibifu wa miundombinu ya maji ikiwemo mabomba ya barabarani.
Pia soma ~ Idara ya Maji nani anawepa maagizo kutoa huduma ya maji usiku wa manane?