Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hayo yameelezwa na Jumanne Abdallah Sagini Agosti 20, 2026 wakati alipokuwa akitoa Mafunzo ya Kujenga Uwezo wa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Songwe kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika Jukwaa la Dira yenye mada ya "Uongozi wa Kimkakati na Mabadiliko ya Fikra Kiuongozi na Kiutendaji katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuwezesha Utekelezaji wa Dira 2050"
"Mabadiliko ya fikra kwetu sote ni injini ya kutufikisha kwenye matokeo tarajiwa na ajenda ya utekelezaji wa Dira 2050 iwe ya kudumu katika vikao vyote muhimu ambapo Utekelezaji wa DIRA utaendelea hata viongozi wakibadilika na wananchi kujiandaa kwa fursa mbalimbali kwani Dira hii ina fursa nyingi kwa kuijua na mikakati ya utelezaji wake wananchi watajiandaa kushiriki na kutumia fursa ziłizopo kukua kiuchumi," ameeleza Mhe. Sagini.