Jumapili tarehe 18, November 2018 Kocha Amunike wa Taifa Stars asiponipangia hiki Kikosi ninachokiamini basi ni bora tu tufungwe na tukose AFCON

Hiki ndo kilikuwa kikosi cha ushindi, yeye anatupangia upuuzi wake tu hapa, aondoke tu kwa kweli
 
Hiki ndo kilikuwa kikosi cha ushindi, yeye anatupangia upuuzi wake tu hapa, aondoke tu kwa kweli

Baada ya Shomari Kapombe Kuumia na kuwa ' ruled out ' kuwa hatocheza leo ' Mtaalam ' wangu akanitumia tena Kikosi cha mwisho na kusema kuwa nafasi ya Kapombe acheze Ramadhan Kessy na namba nane amuache Abubakary Salum ' Sure Boy ' ila kama akimbadilisha na Kumpanga Feisal Toto bado pia ' Kinyota ' tulikuwa vyema kwakuwa hata Wao Lesotho nao walijipanga vyema Kindumba / Kiuchawi wakisaidiwa na ' Waganga / Sangoma ' wengi kutoka kwa Majirani zao Afrika Kusini ila GENTAMYCINE nikaonekana ' natania ' tu. Pengine siku zingine tutaheshimika na kusikilizwa. Wengine hatujaenda huko Maseru Lesotho ila tumepambana Kivyetu kuhakikisha Taifa Stars yetu inaibuka na ushindi leo. Unatupangia Wachezaji wa majaribio sijui Ally Sonso na mwenzake Abdallah Kheri kwanini tusifungwe? Tena hadi nikasema kuwa naomba Kikosi kile watumiwe Watu wa TFF na hasa Benchi la Ufundi nikaonekana ' pomboyo ' fulani hivi.
 
Mtani.GENTA nimekubali leo.

Sitaki mnikubali bali nawataka endeleeni tu Kunidharau na Kuniona ' Pomboyo ' tafadhalini. Mlidhani nilipowapeni tahadhari mapema tena hadi nikawawekeeni Kikosi na kuwaambia ' wafowadieni ' haraka Watu wa TFF na Benchi la Ufundi nilikuwa ' natania ' tu?
 
Chilunda vurugu nyingi saana lakini hafungi!Bado mdogo though....
 
Nipo hapa nalia gentamycin nikiangalia hili pendekezo lako na madudu aliyotufanyia yule shetani mnaijeria sina hamu!
Kwa nn hawakusoma huu uzi?
 
List ilikuwa imetulia sana na tungeshinda tena mengi tu; pale kwa Kapombe alipoumia angejuwa amemwita Shabalala hata sijui kwa nini hakumwita.
 
Nipo hapa nalia gentamycin nikiangalia hili pendekezo lako na madudu aliyotufanyia yule shetani mnaijeria sina hamu!
Kwa nn hawakusoma huu uzi?

Watanzania tuna tabia ya Kudharauliana na Kuchukuliana ' poa ' ila huwa wanakumbuka pale tu mambo yakiharibika. Nimeumia mno Mkuu We acha tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…