Jumapili ya hivi raha sana

Jumapili ya hivi raha sana

Umeamka alfajiri umeingia kwenye nyumba ya ibada hasa ibada ya kwanza kabla ya joto.
Halafu mfukoni una kiasi kidogo cha fedha angalau kununua nyama..kwa maisha yetu nyama tunakula jumapili tu.

Baada ya kununua nyama unarejea nyumbani msosi unaandaliwa. Nachukua kiradio changu pamoja na mkeka, natandika chini ya mti wa muembe pembeni nina dumu langu la mbege na enjoy upepo mwanana unaopoozwa na matawi ya migomba halafu ninasikiliza nyimbo za noten za Kwaya Kuu.


View: https://youtu.be/rJ2pwxpZzGM?si=kSQnFMXU78gdZuUS
Hapo VP

Hayo maisha utayapata pande za Kilimanjaro milimani ni maisha matamu sana.
 
Back
Top Bottom