Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 688
- 1,039
Mungu aibariki Tanzania.
Kwa hiyo ile masters haipo Tena!?
Hii inaonyesha kwamba viongozi wetu (wanaosimamia rasilimali zetu) hawako makini (serious) sana.
Ndiyo maana tunapigwa kwenye mikataba mingi ya uwekezaji kwenye rasilimali zetu. Ndiyo maana kuna mikataba mingi mibovu.
Yaani fikiria chombo kama bunge chenye kazi ya kupitia na kuidhinisha mikataba mingi ya nchi inakosa umakini hata katika mambo madogo kama haya ya elimu ya wabunge, kuhakikisha taarifa zao ni sahihi kabla ya kupakia mtandaoni au kupeleka kwa umma.
Kama hatuko makini katika mambo madogo madogo kama haya basi kuna hatari ya kuendelea kupigwa kwenye mikataba na mambo mengine muhimu kwa taifa.