Ama kwa hakika hali ya jumba bovu aliloliongelea Mama Samia inazidi kudoda:
Siasa ni mchezo mchafu ambao ni muhimu kwa mama kutambua kuwa kuanguashiana majumba mabovu ni sehemu ya mchezo wenyewe.
Inafahamika kuwa wapambe hawajawahi kuwa sehemu ya kuangukiwa na majumba ya namna hii.
Mara zote wao ndiyo wenye kuukaanga mbuyu. Hawaaminiki.
Umdhaniaye siye ndiye!
Yaliwakuta kina Jumbe, Salmin, Lowassa na wengi wengine Dodoma. Walidhani kuwa wengi wakaishia kula na wakwao.
Ikumbukwe, mzee Sitta (rip) alienguliwa kwa kutokuwa mwanamke na ikaishia hapo.
Kwa kujikita kwenye haki, usawa na maridhiano tu Mama angevuna zaidi mno ya urais 2025 katika hali ya sasa.
Hili la Mbowe nalo, wacha tuone litakaye kuja kumwangukia.
Tutakuwapo inshallah, kukumbushana.
----------
Rais Samia, jumba bovu humwangukia wa mwisho