Jumba la Kifahari la Askofu Kakobe

Heheh pole chief. Tusimuasi Mungu, Yeye aweza kutuokoa na wafilisti na majitu. Naam, kuwekeza kujifunza kwa kufundishwa na Roho wa Mungu na ufunuo wa Kristo kwafaa mno. Gal 1:10-12. Siku hizi dini/madhehebu imekuwa biashara kama biashara nyinginezo chief.
 
Umenikumbusha kitabu cha "THE TRIAL OF BROTHER JERO" cha Wole Soyinka
 
Mkuu unatumia Nguvu Kubwa- mno kuhalalisha huu utapeli wa Hawa manabii feki.

Nauita utapeli maana tapeli hakulazishi kabisa kutoa pesa na pesa unaitoa mwenyewe.

Ila mwisho wa siku hatoibadili tasfiri ya neno utapeli kua Ni KUJIPATIA PESA KWA NJIA ZA UDANGANYIFU
 
Alikudanganya nini?
 
Wapi huko? Ona wanavyoishi maisha ya kifahari wakati waumini wao wanaishi maisha ya kikapuku
Acha mawazo mgando wewe!!!
Ukiwa na duka wateja wakiwa wengi na kutengeneza faida ndo uogope kufanya mambo yako kisa tu itaonekana una maisha mazuri kuliko wateja wako?

Na hujuilizi tu,kwanini tunaaminishwa Mungu ndo kila kitu lakini yatupasa kutoa sadaka na zaka?
Kwanini wanatuombea ila mwisho wa siku wataangalia tumeweka nini kwenye box la sadaka?

Dini ni biashara,so ikilipa matokeo yake ndo hayo.
 
Ila waumini wake hata kulipa kodi ya chumba kimoja cha kupanga cha giza, Tsh 20,000 kwa mwezi huko Buza kwa mama kibonge hawawezi.
Ni ngumu kuweza coz,fikiria,wewe huna hata 100,lakini umeweza kuorganize watu wakakupa kidogokidogo ukapata elfu 50. Kwavyovyote,wewe utakua na hela,ila wale walokuchangia bukubuku yawezekana akawa amebaki na zero,au jero.
So kwa vyovyote anaekusanyiwa lazima awe nazo.

We unasema chumba,yawezekana kuna wanaokufa njaa,lakini mchungaji au askofu lazima apate sadaka yake Mkuu.
 
Ulichoandika hapa, Yesu alikisema kuhusu Mafarisayo na Walimu wa sheria. Soma Mathayo sura ya 23 na 24.
 
Mungu kamwinua....nawe mtumikie bwana ...utafanikiwa zaidi
 
Mboba unatoa mfano wa kipuuzi, ilo duka majirani wamekusaidia mtaji.
 
Mboba unatoa mfano wa kipuuzi, ilo duka majirani wamekusaidia mtaji.
Kwani na nyie Kakobe mlimsomesha?
Mlimpa nyie wazo la kuanzisha kanisa?
Huwa mnaisadia kuingiza ibada?
Huwa mnamsaidia kuhubiri?
Alishawahi kuwafuata majumbani muende kanisani kwake?
Alishawahi kuwakaba mtoe sadaka?
Mliwahi kumsaidia kujenga kanisa?

Huo ndo mtaji wake kama ulivyo kwa mwenye duka.
Acha wivu wa kike,pambana na hali yako.
Tuliza hasira kwenye maendeleo ya wenzio,vinginevyo stress zitakuua Dunya wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…