Jumbe aeleza alivyofuatwa na Wasafi kumuomba wimbo wake "Siri"

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Vichwa vya wasafi group kwa sasa vimejaa starehe tu na vinafikria ngono na pombe. Hawawezi kujishughulisha kutunga tena wimbo kwa kutumia vichwa vyao kama ilivyokuwa zamani. Alianza kubwa lao Diamond kudokoa na kurudia nyimbo za wasanii wengine ili kujipatia kipato, sasa hata wasanii walioko chini yake wameiga mtindo.

Na wao ni mwendo wa kurudiarudia nyimbo za wasanii wengine aka kuidokoa dokoa nyimbo za wengine

Jumbe amesema kuwa alifuatwa na timu ya wasafi wakiongozwa na Babu Tale na walikubariana na amekiri kulipwa vizuri ili Ray Van aweze kutuimba wimbo wake " Siri"

Wasafi punguzeni starehe LA sivyo mtapotea
 
kweli hata Haleluya,Waka Diamond ameiga pia....
 
Mkuu mbona ni jambo la kawaida na ushukuru amelipwa. Jay D kwenye ubora wake aliimba Muhogo wa Jang'ombe wa bi kidude na hakuna aliepiga kelele sikumbuk kama alilipwa yule Bib
Ila kwenye Tasnia ya Music hilo ni jambo la kawaida sana kwa wanamuzik kurudia nyimbo za wanamuzik wa zaman kwa makubaliano maalumu na sio kuishiwa
 
Sio Muhogo wa Jang'ombe tu bali pia aliimba Siwema ya Marijani Rajabu.
 
Mh walimwengu siku hizi mmejaa majungu na fitina.wanarudia kina Chris brown mambefenge huko hamneni ila mbongo mwenzenu nongwa.

Punguzeni husda,watu sa hivi wanahangaika mkono uende kinywani we umekalia majungu.we kama hupendi watasikiliza wengine
 
Yap, labda Rayvan na Harmo lkn mtu na dadayake hakunaga chamaana wanachoimba, watoto wa uswahilini waishia kusifia video zao. Wanakimbilia kutoa video ili kufunika mapungufu ya audio. Mondi hana mashairi ya kufikiria kwa sasa, anafanya biashara huku kila kukicha anawaza aimbe na nani wa nje ya nchi bila hata kuwaza anachotaka kukiimba. Sikiliza, Nana,Fire,waka, labda merry you inaonekana km alijiandaa. Hata km ni miziki ya club basi someni lyrics za kina shaggy, sean paul au beanman mbona wao wanapangilia vzr
wanachokiimba. Unakuta nyimbo unaimba kitu kile kile mara moyo wangu, mara kulewa. New msg ni kitu kizuri kwa mwanamzk lkn wetu hapa wanabdilisha title tu za nyimbo. Mwana FA ni mwanamzik wa mfano sn, ni km anafanya research ya nini kilichoko mitaani ndo anakuja na ngoma. Hipop kwa ujumla wapo vzr, bongoflava ya sasa bora usikilize singeli utakutana na mashairi yaliyo tulia.
 
Mtoa mada unasumbuliwa na wivu na umasikini. Watanzania tunakuwa na roho mbaya na roho ya korosho kwa waliofanikiwa.
Katika watu unaodai wanarudia nyimbo umewaona wasanii wa wasafi tu? Hivi mtu akisema waka waka utasema kaiba wimbo. Akisema Haleluya nayo kaiba wimbo?

We ni mpumbavu tu, kasikilize wimbo wa Ali Kiba ''Kimasomaso'' urudi hapa.
 

Kina Diamond ni New School, so ili kutukamata Old Schools ni kwa style za namna hii. Naamini akiurudia vizuri wimbo ulioimbwa na mkongwe itatukumbusha nyuma.

Na most likely tunaweza kushushia bia.
 
Tunakunjiana wenywe kwa wenyewe
Jamaa ndo washaukata ata tukikunja haina maana tupambane tu na hari zetu
 
Sa hivi ukisikia WCB wanarelease ngoma mpya hamna hata ile hamu ya kusubiri kusikiliza wameimba nini
No creativity at all
 
kaka ile
kimasomaso ilikuwa project ya kusaga kipindi ambacho wasanii wengi walirudia ngoma za kale tuliza mshonoooo acheni kuigiza ngoma fanyeni kazi.
 
Wengine muziki wenyewe wamejulia ukubwani...

Jide wakati akiwa bado hot, pamoja na Muhogo wa Jang'ombe na pia alirudia Siwema, let alone Ndindindi aliyoifanya mwishoni akiwa amepunguza speed!!!
 

Samahani Mtarban, wewe ni he or she? Kulikoni hSimba na Wasafi huwa wanakushughulisha sana? Kuna wakati nilikuwa nakuhisi wewe ni Mobeto,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…