Jumia na tabia ya kuchomoa vifaa kwenye bidhaa wanazouza

sontable

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2018
Posts
261
Reaction score
535
Jumia ni kampuni ya kuishtaki tu kwa sababu wanapouza bidhaa zao huwa wanachomoa baadhi ya vifaa na vinafika vikiwa sio complete ukilinganisha na ungenunua dukani.

Pia ukijaribu kuwapigia katika namba zao mara hawapatikani mara huwezi kuunganishwa kwa sasa mara wakipokea wanakujibu ili mradi tu wanakufariji lakini nothing to help you mpaka saivi nina mabidhaa yao sina hamu nayo na nimenunua vitu more than 4 million kwao ila sioni wakinijali.

Mfano nilinunua camera haina memory na wakati huohuo wapo walionunua dukani ina memory na bei chini ya niliyonunulia mimi,na vingine vingi.

Sitaki hata kuwasikia hawa viumbe

JUMIA HATA KAMA NI UDALALI HATUFANYI HIVYO!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nchi zetu hizi biashara bado sana aisee! Yaani hao wanaoagizwa kuleta sio waaminifu mkuu!
Ni sawa na kule bandari zamani (sijui kwa sasa) walivyokuwa wanachomoa vitu kwenye magari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana, labda huo utapeli wameanza sikuhizi, ila Mimi kwa uzoefu wa kununua bidhaa zao,ziko Imara nilinunua friji na pasi mwaka jana mwanzoni mpka Leo zinapiga kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jumia walishaacha kuuza vitu, now wanafanya kazi kama ebay, mfanyabiashara anaweka vitu vyake jumia, unaponunua kitu kinatoka kwa mfanya biashara kuja kwako.

Kifupi siku hizi ni pango la madalali wananunua vitu kariakoo na kuja kuviuza jumia kwa faida.
 
Wewe umetumwa nawashindani wa kampuni ya jumia uje kuichafua kampuni hii

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa akili zako ndo unafikiri hivyo siijui kampuni yoyote inayoshindana na jumia zaidi ya kupatana lakini kupatana hawauzi wao wanaouza ni wateja kwa wateja nako vitu ni vibovu vilevile


Kinachoniumiza zaidi ni pale ambapo wameniuzia bidhaa afu bidhaa yenyewe imekuja haina vitu vyote na nimewapigia simu sana lakini majibu wanayonipa ni ya kisengerema kweli na ni waongo haijapata kutokea nina document zao zote hapa nilipo nasubiri kuwaniga mahakamani maana wamenitia hasara tu

Nachotaka kusema dont trust online bussness bidhaa nzuri na halisi ni ile unayoenda kununua mwenyewe dukani

Kwanza picha ya bidhaa unayowekewa kwenye app yao na bidhaa jinsi ilivyo ni vitu viwili tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani Jumia unalipia kabla ya kuiona bidhaa au baada ya kuiona bidhaa eti...?
 
Nunua vitu aliexpress wapo vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…