Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) yakemea vitendo vya utekaji, ukatili na mauaji yanayoendelea nchini

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) yakemea vitendo vya utekaji, ukatili na mauaji yanayoendelea nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imekemea vitendo vya utekaji, ukatiili na mauaji yanayofanywa na genge la watu wasiojulikana na kulaani tukio la kuchukuliwa na kuuawa kikatili kwa kada wa Chadema, Ally Kibao.

CCT ni Taasisi inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotestanti pia inaundwa na makanisa mbalimbali wanachama na vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Tayari Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na mauaji hayo na kuagiza vyombo vya uchunguzi kumpelekea haraka taarifa ya kina juu ta tukio hilo na mengine ya aina hiyo.

Katika ujumbe wake kwa Mwananchi jana usiku, Septemba 8, 2024, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Fredrick Shoo amesema sasa ifike mwisho kwani inaumiza kila kukicha kusikia taarifa za watu kutekwa, kufanyiwa ukatili na kuuawa na watu wasiojulikana.

“Watanzania tumefika huko? Ndio njia tumeamua kuiendea? Hao wafanyayo hayo sasa wanaonyesha wazi, tena mchana kweupe kuwa hawamwogopi yeyote, chochote, wala hawana hofu ya Mungu tena,” amesema Askofu Shoo na kuongeza.

“CCT tumesikitishwa sana na mauaji na ukatili wanaofanyiwa Watanzania wasio na hatia. Tunakemea vikali utekaji, ukatili na mauaji yanayoendelea nchini kwa sasa.”

“Mnaofanya hayo iwe ni kwa sababu yoyote ile, mjue yupo Mungu, nasi tutamwomba adhihirishe wazi uwezo na mamlaka yake. Mungu hadhihakiwi,” amesema.

"Kama mnayafanya hayo ili kuwajaza watu hofu, jueni Watanzania tunasema kwa haya hatuogopi wala hatutaogopa. Tunayakataa, kuyapinga na kuyakemea wazi,” amesaema Askofu Shoo ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT.

Katika maelezo yake, kiongozi huyo wa kiroho amesema: “Kama lengo lenu ni kumchafua Rais wetu ili mikono yake ijae damu za watu, jueni kuwa mmeshashindwa na mtashindwa vibaya, kwa maana Mungu atatenda jambo."

Mkuu huyo wa KKKT mstaafu amesema: “Tunatoa wito kwa Watanzania wote waombe kwa dhati na kukemea vitendo hivi viovu vinavyotaka kutishia usalama, haki na amani kwa raia wa nchi yetu."

MWANANCHI
 
Nipende kusema usalama wa taifa lolote lile ni pamoja na ustawi na furaha ya jamii katika taifa husika na taswira ya mahusiano kimataifa.

Yeyote aliyeshauri kuanzisha project ya kuwateka na kuua raia hajaisaidia serikali lakini pia Sinto fahamu anayo/ wanayo itengeneza ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa.

Ni dhahiri wanaotekeleza mambo hayo maovu dhidi ya raia Japo wanafanya nje ya mfumo rasmi wautendaji, wanajulikana ila wanalindwa kwa sababu tusizo zijua hasa kwa sasa.

Niseme tu, duniani kote machafuko huanzishwa na hizo rogue elements. Hivyo wanaoendesha utekaji na mauaji ya raia wanahatarisha usalama wa taifa, ustawi wa jamii iliyostaarabika, kuichafua serikali kitaifa na kuichafua inchi kimataifa.
 
Hao wanaotekekeza uhalifu huo, wanadhsni kuwa ndiyo wanakisaidia chama Tawala!😳
 
Back
Top Bottom