Jumuiya ya Kikristo: Tulikosa Kibali kushiriki Uchaguzi mkuu 2020

Jumuiya ya Kikristo: Tulikosa Kibali kushiriki Uchaguzi mkuu 2020

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo Rais Samia Suluhu ameshiriki kwenye Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo na miongoni mwa maombi yao ni kushiriki kwenye Demokrasia na Chaguzi.

Jumuiya hiyo imesema ushiriki wa taasisi katika uchaguzi wa kidini haukuwepo kabisa kutokana na kukosa kibali kutoka mamlaka husika na wanaomba wahusishwe zaidi mbeleni.

Pia Jumuiya imepongeza utawala sheria kwenye awamu ya sita ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa Serikali waliokuwa na tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka na kuminya haki za msingi za binadamu.

TUME YA UCHAGUZI ilibana had I makanisani?
Kwa upande mmoja nadhani Mungu alikusudia viongozi wa dini waepushwe na dhuluma.

Akanyakua aliyeamuru wizi
Afadhali hawa wamejaribu kuchokonoa kwa mbali suala linalohusu maisha ya raia tofauti na wale wanaofikiri kuwa dini inapaswa kujihusisha na mambo ya kiroho tu.

Hakuna roho bila mwili au mwili bila roho. Vyote hivi vinategemeana na kutunzwa kwa usafi wa mwili na roho. Ukiona udhoofu na makunyanzi ya mchoko kwenye mwili wa mtu jua wazi kuwa hili ni jawabu la hofu na fadhaa ya roho.
 
Leo Rais Samia Suluhu ameshiriki kwenye Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo na miongoni mwa maombi yao ni kushiriki kwenye Demokrasia na Chaguzi.

Jumuiya hiyo imesema ushiriki wa taasisi katika uchaguzi wa kidini haukuwepo kabisa kutokana na kukosa kibali kutoka mamlaka husika na wanaomba wahusishwe zaidi mbeleni.

Pia Jumuiya imepongeza utawala sheria kwenye awamu ya sita ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa Serikali waliokuwa na tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka na kuminya haki za msingi za binadamu

Wanamwambia nani sasa. Hao wajasiriamali wa dini
 
Leo Rais Samia Suluhu ameshiriki kwenye Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo na miongoni mwa maombi yao ni kushiriki kwenye Demokrasia na Chaguzi.

Jumuiya hiyo imesema ushiriki wa taasisi katika uchaguzi wa kidini haukuwepo kabisa kutokana na kukosa kibali kutoka mamlaka husika na wanaomba

Wasipewe kibali kabisa. Hawa watatumia hicho kivuli kuleta mambo yao ya udini. Hizi dini za siku hizi zinalazimisha madaraka na nafasi. Kuna shida gani?
Tanzania kila mtu ana dini yake ila Taifa letu halina dini maalumu
 
Mie wananichanganya, somebody please explain to me kuna wale waliokuwa wamejikusanya Dodoma walikuwa ni viongozi wa makanisa ya kikristu ndio Hawa au nini?

Kama sio hawa basi wale wahuni wakae kimya maana walikuwa busy kumsifia bwana yule. Na walishiriki vizuri tu.
 
Wale ni kanisa la Assemlis of God.
Leo ni miongoni mwa makanisa ya kikristo(umoja kihuduma)
Hao unaowasema bado hawajajiunga kwa orodha iliyotajwa Leo.
NB wana Uhuru wakujiunga na CCT.
umeelewa?kazana kutoa sadaka ubarikiwe
 
B
Leo Rais Samia Suluhu ameshiriki kwenye Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo na miongoni mwa maombi yao ni kushiriki kwenye Demokrasia na Chaguzi.
Bora hamkushiriki vinginevyo mngeshiriki dhambi na Laana kubwa .
 
Jumuiya hiyo imesema ushiriki wa taasisi katika uchaguzi wa kidini haukuwepo kabisa kutokana na kukosa kibali kutoka mamlaka husika na wanaomba wahusishwe zaidi mbeleni.
mwendazake kaondoka na tuhuma nyingi za kuminya haki za binadamu.
 
Kwani viongozi wa dini wanataka kushiriki vipi kwenye siasa? Kama wanapenda siasa, wachague moja, waachane na dini. Biblia inasema, huwezi kuwatumikia mabwana wawili, ama utampenda zaidi huyu na kumchukia mwingine. Wachukue mfano kwa Askofu Mpango aliyekua Askofu wa Kanisa Anglican, Dayosisi ya Western Tanganyika aliyeamua kuacha Uaskofu akagombea Ubunge huko Kasulu.
 
Nataka katiba ya kuleta haki tu , sitaki kingine
muwe mnatumia akili siyo matope haki gani unayoitafuta ambayo haipo kwenye katiba hii hivi mnafikiri mawazo ya kila mmoja raisi awe anayatumia kuendeshea nchi anaweza kweli hata kama ungekuwa wewe huyu akisema hivi unafanya mwingine akisema hivi unafanya huo siyo urais
 
Hatutaki mawazo ya mtu mmoja mmoja ndio maana tunataka katiba ya Warioba
 
Back
Top Bottom