Jumuiya ya Madola yaendelea kuibana Tanzania yataka hatua zaidi

Jumuiya ya Madola yaendelea kuibana Tanzania yataka hatua zaidi

Baada ya miezi 18 kutokq sasa .....Samia na wahuni wote wataanza kuchanganyikiwa ...shikeni haya mqneno yangu ....HATARI KALILI NA HOFU ITAKUWA JUU YAO... KWA SASA HIVI BADO WAMEPOFUCHWA NA PESA NA NGUVU ZA UONGOZI... NARUDIA TENA BAADA YA MIEZI 18 KUNA ANZA KUPAMBAZUKA KWA UPANDE WA HAKI NA UPANDE WA WAOVU KUNAANZA KUINGIA GIZA....Wazanzibar jiandaeni pia..kama mnayo chembe yq akili bqsi akikisheni muungano unavunjika kabla ya kuwa too late.
 
Kwa hyo tuwaachie wahalifu wote magerezani au sijaelewa. wakati wa utawala wa wajerumani uhaini ilihusisha mauaji ya jamii nzima. Leo Tz tunanyonga m1 imekua nongwa.
Hapqnq ..Bali Wahalifu wote waliopo Ikulu waanze kujipeleka jela wenyewe kutumikia uovu wao
 
October 29 haijaisha hadi iishe.

Bado tupo na wauaji sana , na muda unavyoenda watachagua njia rasmi au zisizo rasmi.

Hatutasamehe wala hatutasahau.
 

Kundi la Mawaziri wa Jumuiya ya Madola la Kuchukua Hatua (CMAG) limeamua kuendelea kuiweka Tanzania kwenye Ajenda Rasmi (Formal Agenda) ya kundi hilo, huku likitaka Serikali kuchukua hatua zaidi katika kuimarisha maridhiano, uhuru wa kiraia na kisiasa pamoja na uwajibikaji.

Uamuzi huo umetolewa katika kikao cha 74 cha CMAG kilichofanyika Septemba 20, 2026, New York, Marekani, pembeni ya Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa yake ya mwisho, CMAG ilisema imezingatia maendeleo yaliyofikiwa Tanzania katika baadhi ya maeneo, lakini ikasisitiza kuwa bado kuna haja ya kufanyika kazi zaidi ili kufanikisha mchakato jumuishi na wenye uaminifu wa mazungumzo baina ya vyama vya siasa.

Kundi hilo pia limetaka kuendelea kulindwa kwa uhuru wa kiraia, kisiasa na vyombo vya habari, pamoja na kuhakikisha taratibu za haki, kwa wakati na kwa uwazi katika kesi ambazo bado hazijamalizika.

Aidha, CMAG imetaka kuwepo kwa taratibu zinazoaminika za uwajibikaji, kupata haki na fidia stahiki kwa watu walioathirika.

CMAG ilikumbusha masharti manne iliyoyaainisha katika mkutano wake wa 71 wa Desemba 2025, pamoja na matarajio yenye muda maalumu yaliyowekwa katika mkutano wake wa 73 wa Julai 2026.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa Tanzania itaendelea kufuatiliwa na CMAG, huku kundi hilo likitarajia maendeleo zaidi katika maeneo yaliyotajwa.

Katika taarifa hiyo, CMAG pia ilisema ilifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, John Palamagamba Kabudi.

CMAG ilitambua ushirikiano wa Tanzania na Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, pamoja na mazungumzo ya hivi karibuni na vyama vya siasa na hatua kuelekea maridhiano Zanzibar, ikisema mambo hayo yanaweza kuwa msingi wa maendeleo zaidi.

Kundi hilo limetoa wito kwa Serikali ya Tanzania kukubaliana mapema kuhusu ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ili aweze kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na wadau wengine.

Pia limekubali Tanzania kubaki kwenye Formal Agenda na kumwalika Katibu Mkuu kuendelea kushirikiana na nchi hiyo, kutembelea Tanzania na kutoa taarifa kuhusu maendeleo pamoja na maeneo ambayo Tanzania inaweza kuhitaji msaada wa kitaalamu kutoka Jumuiya ya Madola.

Soma pia: Haya hapa madhara kwa Tanzania endapo haitatekeleza masharti ya Jumuiya ya Madola

CMAG pia ilifanya mazungumzo kuhusu Uganda na kuamua nchi hiyo ibaki kwenye ajenda rasmi, huku ikiitaka Serikali ya Uganda kuimarisha utawala wa kiraia na kikatiba, kulinda nafasi ya kiraia na vyombo vya habari na kuheshimu taratibu za haki.

Kikao kijacho cha kawaida cha CMAG kinatarajiwa kufanyika Novemba 2026 nchini Antigua na Barbuda, pembeni ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM), ambapo kundi hilo pia litawasilisha taarifa yake ya kila baada ya miaka miwili kwa wakuu wa Serikali.
Hakuna la maana hapo. Maneno meengi yasiyo na vitendo.

Kelele tu. Huku madhara, vifo, kesi na wanaotekwa wanaongezeka.

Wazungu wanatafuta fursa tu na sio vinginevyo . Uharamia wetu ni mtaji kwao.

Watakuambia umeharibu demokrasia, sasa tupe hiki na hiki ili na sisi tukupe misaada. Madini yako hatarini, mbuga, nk
 
Hawa wanafanya sehemu yao kwa kadri inavyowaruhusu; lakini kazi ni yetu sisi wenyewe.

Tatizo ni kuwategemea wao kuwa watatuletea mabadiliko tunayoyataka. Hilo haliwezekani.
 
Back
Top Bottom