Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
YAH: TAARIFA KWA UMMA.
Mosi, Tangazo la Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Chuo Kikuu Dar es Salaam ndugu Goodluck Evarist la kuwataka wanafunzi ambao hawajapata mkopo na walio na mkopo mdogo wawe na kadi ya Chama ili wasaidiwe, sisi DUPSA tunalaani Tangazo hilo la kibaguzi lenye lengo la kutugawaya hivyo tunaungana na taarifa ya bodi ya mkopo (HESLB) la tarehe 13/08/2024 kupinga kauli hiyo.
Pili, Tunalaani Tangazo la DARUSO MLIMANI kupitia wizara ya Habari, sayansi na teknolojia la tarehe 14/08/2024 la kuzuia wanafunzi kutoka na kupokea taarifa kwani ni kinyume cha katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18(1) na (2). pia ni kinyume cha katiba ya DARUSO Mlimani ibara ya 1(v). Hivyo Tangazo hilo lipuuzwe.
Tatu, Tunalaani na kupinga kauli zote za kibaguzi, kichochezi na zenye lengo la kutugawanya, kusambaza chuki au kuminya haki za msingi za watu zinazotolewa na viongozi wa DARUSO Mlimani na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa kwani ni
kinyume cha falsafa ya Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 4R. Aidha, DUPSA inawataka wanafunzi, viongozi wa DARUSO Mlimani na vyama vya siasa kufuata Katiba, sheria, taratibu, kanuni na miongozo tuliyonayo iliyopo chuoni. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki DUPSA Asanteni.
Pia soma:
~ Wanafunzi UDSM tuliokosa mikopo 2023 na waliopata mikopo kidogo tunaambiwa lazima tuwe na Kadi ya CCM ndio tutahudumiwa
~ HESLB yafafanua madai ya Wanafunzi UDSM kutakiwa kuwa na Kadi ya CCM ili wapate mkopo