Kigogo kesharusha hii document mitandaoni!!
Hapo kwenye kutoa ripoti hadharani,kuna watu inabidi tu wakubali kishingo upande.
Hata kama itakuwa ni kusamehewa kulipa madeni kwa muda huo kutokana na athari za corona kiuchumi, nafuu hiyo inaweza kutumika zaidi katika kujenga miundombinu na si kugusa moja kwa moja maisha ya watu maana awamu hii inathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko watu unless unafuu wa kulipa madeni uendane na mashariti maalumu kuhakikisha wananchi wananufaika nao moja kwa moja.
Kwa mfano,kwa hapa nchini,serikali inatakiwa kutumia unafuu huo wa kulipa madeni(kama utatolewa) ama kwa kuongeza mishahara ya watumishi au kulipa madeni yao,kufidia sekta zilizoathirika na covid kama utalii,n.k.