Juni 10 IMF & World Bank kuamua iwapo Tanzania tunakidhi kupewa mkopo tulioomba kupambana na corona au hatustahili

Juni 10 IMF & World Bank kuamua iwapo Tanzania tunakidhi kupewa mkopo tulioomba kupambana na corona au hatustahili

Ukilia njaa kwa wananchi walkout huo ni udhaifu kwa kiongozi. Inabidi upambane kwa kila mbinu kuhakikisha chakula kinapatikana.
Huwezi lalamika kwa wanao chakula hakipo wakati uko na jinsi ya kupata chakula huo ni uzembe. Hata kwa kuiba unawezafanya ili kuokoa familia na kufedheheka.
Sahihi kabisa kwa family level hasa kama watoto bado wadogo ila kama ni vijana watu wazima wanaoelewa hali ikoje njia bora ni kuwaambia ukweli wote. Uongo hautasaidia.
 
Tafakuri ya Dr. A. Lwaitama - Tanzania vita yake dhidi ya CORONA ni siasa na siyo ya kisayansi

  • Tanzania haikuwa na uwezo wa kuwalisha watu wa mijini hivyo iliweka lockdown ya kinamna yenye mrengo wa kisiasa
  • Asilimia 70% ya watanzania wanakaa vijijini ambapo wanajitegemea kwa chakula , mitishamba kama alovera na majani ya nyungu
  • Maamuzi ya Tanzania yaliangalia uhalisia serikali haingeweza kuwalisha watu wa mjini, hivyo kuamua kuja na lockdown ya kisiasa kuonesha inawapenda na kuwajali watu
  • Lockdown ya ulaya haikuwa total lockdown watu waliruhusiwa kwenda supermarket, pharmacy kwa utaratibu maalum
  • Lockdown za ulaya na Tanzania kufunga vyuo, kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuzuia mikusanyiko zote zilikuwa za kisiasa zaidi maana hazikuwa za kiimla kama China, Vietnam , Rwanda n.k

Je andiko la serikali ya Tanzania kuomba ahuweni ya mikopo toka IMF / World Bank limezingatia hilo au wame kopi na kupesti toka nchi zilizoona mbali kama za Rwanda, Uganda na Kenya kuendelea kuipiga vita Covid -19 kwa kutoa takwimu, mass testing / kulazimisha upimaji kwa wote bila kujali wana dalili au hapana za covid-19, kufuata makubaliano ya kubadilishana taarifa, kuzingatia miongozo ya WHO / CDC / AU/ EAC / SADC n.k ikiwemo total lockdown, partial lockdown na ile ya mchanganyiko wa curfew& lockdown ?
 
Tanzania tumeomba tusamehewe chini ya hiyo relief programme ili tupate pesa ya kutusaidia kupata vifaa tiba vya kupambana na corona.

Kwenye barua yake ya kuomba serikali imesema imeshindwa kufanya vipimo na kufuatilia muenendo wa corona kwa sababu ya ukosefu wa pesa.
Mkuu Mfukua Makaburi, kwanza asante kwa taarifa hii toka IMF.

Nina kaswali kamoja kadogo, katika barua hiyo ya IMF, hakuna popote walipoeleza hoja za serikali yetu kuomba msaada huo!, sasa hizo hoja kuwa Tanzania tumeshindwa kuwapima Corona watu wetu kwasababu ya ukosefu wa fedha, umezitoa wapi?!
P
 
Hii nchi imejaa wendawazimu. Unaombaje msaada wa kupambana na kitu ulichoitangazia dunia mmeimaliza tena kwa maombi.

Mi nadhani kwa kuwa Mungu wa Tanzania na Afrika anatuoenda sana tuombe kila kitu kwake.

Tuachane kabisa na hawa mabeberu.
 
Kigogo kesharusha hii document mitandaoni!!

Hapo kwenye kutoa ripoti hadharani,kuna watu inabidi tu wakubali kishingo upande.

Hata kama itakuwa ni kusamehewa kulipa madeni kwa muda huo kutokana na athari za corona kiuchumi, nafuu hiyo inaweza kutumika zaidi katika kujenga miundombinu na si kugusa moja kwa moja maisha ya watu maana awamu hii inathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko watu unless unafuu wa kulipa madeni uendane na mashariti maalumu kuhakikisha wananchi wananufaika nao moja kwa moja.

Kwa mfano,kwa hapa nchini,serikali inatakiwa kutumia unafuu huo wa kulipa madeni(kama utatolewa) ama kwa kuongeza mishahara ya watumishi au kulipa madeni yao,kufidia sekta zilizoathirika na covid kama utalii,n.k.
Haituhusu, Sisi tumekubali Mziki wa JPM 2020 . Mungu Mlinde Rais wetu mwenye Mapenzi Mema na nchi yetu.
Nimecheka sana baada ya kusoma Write up ya Zitto Kabwe. Hivi Zitto Kabwe anaweza kuongelea ni nini Mwaka 2020.
 
Mkuu Mfukua Makaburi, kwanza asante kwa taarifa hii toka IMF.

Nina kaswali kamoja kadogo, katika barua hiyo ya IMF, hakuna popote walipoeleza hoja za serikali yetu kuomba msaada huo!, sasa hizo hoja kuwa Tanzania tumeshindwa kuwapima Corona watu wetu kwasababu ya ukosefu wa fedha, umezitoa wapi?!
P
Mkuu p.

Kwenye post namba 20 nimeweka barua ya Tanzania kuomba mkopo ya May 27, 2020. Pitia post namba 20 mkuu.

Ahsante.
 
Nobody can bring us to our knees,Tanzania is a Sovereignty State.
Only money can bring us to our knees.

Money has brought us into our knees. We are now kissing beberus ass for money.

There is no such thing as sovereignty for a poor country. As long as you are poor you are not a sovereign country.

Don't be fooled by politicians. They can say anything for political reasons. They can promise you that stones can be cooked while in fact you can't cook stones.

You can see now what happened, we have been told that we can't bow down for anyone for money as we are self sufficient but behind closed doors our top officials are kissing beberus as for money.
 
Zitto hajaandika barua ya kuomba tunyimwe hiyo nafuu?
Nafuu tuliomba April ,wao wanakaa june 10,tumeshapita kwenye hali ngumu,watupe wasitupe haitatuathiri kama nchi
Kenya walikubali lock down,wamelamba usd 1 bilioni fasta,bila vikao vya bodi,kazi itakua kuirudisha baada ya corona kwisha
 
Post number ishirini ya uzi huu, mbona sahihi ya Waziri na Gavana zinafanana ama macho yangu!!? Barua itakuwa fake hii nini?
 
Zitto hajaandika barua ya kuomba tunyimwe hiyo nafuu?
Nafuu tuliomba April ,wao wanakaa june 10,tumeshapita kwenye hali ngumu,watupe wasitupe haitatuathiri kama nchi
Kenya walikubali lock down,wamelamba usd 1 bilioni fasta,bila vikao vya bodi,kazi itakua kuirudisha baada ya corona kwisha
Hiyo ya April umeitoa wapi?

Nimeweka barua ya May 27 ya serikali kuomba msaada na sio April.

Kwenye barua serikali inasema kuanzia july itakua na hali mbaya sana.

Soma post no 20.
 
Zitto hajaandika barua ya kuomba tunyimwe hiyo nafuu?
Nafuu tuliomba April ,wao wanakaa june 10,tumeshapita kwenye hali ngumu,watupe wasitupe haitatuathiri kama nchi
Kenya walikubali lock down,wamelamba usd 1 bilioni fasta,bila vikao vya bodi,kazi itakua kuirudisha baada ya corona kwisha
Kuna Shida mahali... Mnasema barua iliandikwa April, lakini mnayoonyesha hapo (post #20) ni ya May 27. Tushike lipi!?
 
Back
Top Bottom