Juni 10 IMF & World Bank kuamua iwapo Tanzania tunakidhi kupewa mkopo tulioomba kupambana na corona au hatustahili

Hakuna saini hapo. Toa 10000 mpya uangalie saini
Post number ishirini ya uzi huu, mbona sahihi ya Waziri na Gavana zinafanana ama macho yangu!!? Barua itakuwa fake hii nini?
 
Kigogo kesharusha hii document mitandaoni!!

Hapo kwenye kutoa ripoti hadharani,kuna watu inabidi tu wakubali kishingo upande.

Hata kama itakuwa ni kusamehewa kulipa madeni kwa muda huo kutokana na athari za corona kiuchumi, nafuu hiyo inaweza kutumika zaidi katika kujenga miundombinu na si kugusa moja kwa moja maisha ya watu maana awamu hii inathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko watu unless unafuu wa kulipa madeni uendane na mashariti maalumu kuhakikisha wananchi wananufaika nao moja kwa moja.

Kwa mfano,kwa hapa nchini,serikali inatakiwa kutumia unafuu huo wa kulipa madeni(kama utatolewa) ama kwa kuongeza mishahara ya watumishi au kulipa madeni yao,kufidia sekta zilizoathirika na covid kama utalii,n.k.

Kwani shida iko wapi kama zitaenda kujenga miundombinu? Kila nchi imeathilika na corona iwe kwa wagonjwa au kiuchumi, hivyo hili ombi aliliomba Raisi magufuli kwa hiyo kama itafanyika basi itakuwa sahihi,

kumbuka hilo jambo alilizungumzia barozi wa ufaransa hapa kwetu na akasema wanashauliana na taasisi zingine ili jambao hilo liweze kufanyika kwa hiyo sio taarifa ya kigogo,
Mpaka sasa kama taifa tumepungukiwa huduma za hospitali kwa sababu ya corona,huduma zingine zinakwama kwa upungufu wa kifedha, hivyo pesa za bajeti ya miundombinu huenda ilitumika kwenye corona kwa hiyo si mbaya hiyo pesa ikitumika hapo.
 
Korona imeshaisha
Mkopo wa nini?
Tunakwenda kuongeza deni la taifa kwa tatizo hewa lisilokuwepo

Hakuna mkopo unaotakiwa hapo, bali ni kusitishwa kwa kulipa deni kwa muda, ila ukifata taarifa za watu humu na huyo kigigo utachemka, mara serikari ipewe mkopo mata isitishiwe deni sasa lipi ni hitaji lao?
Tatizo account ya kigogo wanaoiendesha wamechanganyikiwa kwa sasa kila mtu anaandika tu kupunguza stress walizonazo.
 
Kama Korona imeisha huwezi kuitumia korona kama kisingizio cha kusitisha mkopo, Watafute kisingizio kingine chenye mashiko.

Watu mtaani hata barakoa hawavai tena, sasa hiyo korona ya excuse ya kuombea usitishiwe mkopo iko wapi?
 
June 10 bodi ya wakurugenzi wa shirka la fedha Duniani na Bank ya Dunia kuamua iwapo tunastahili kupewa msamaha na mkopo kupambana na corona au laa.

Mwezi April IMF na WB walitengeneza kitu kinaitwa Catastrophe Containment and Relief Trust ili kusaidia nchi masikini kupambana na madhara ya corona.

Kwenye hiyo relief programme nchi masikini zitasamehewa kulipa madeni yake hadi miaka 2.

Tanzania tumeomba tusamehewe chini ya hiyo relief programme ili tupate pesa ya kutusaidia kupata vifaa tiba vya kupambana na corona.

Kwenye barua yake ya kuomba serikali imesema imeshindwa kufanya vipimo na kufuatilia muenendo wa corona kwa sababu ya ukosefu wa pesa.

IMF imesema June 10, 2020 bodi itaamua kama tunakidhi vigezo kusamehewa au lah.

Soma barua ya IMF kwa serikali.View attachment 1469742
Hatustahili, Tanzania hakuna corona, hizo fedha akizipata dotto itaingizwa kwenye mradi wa kuendelea kununua wapinzani.
 
Walienda kutambika gamboshi ili corona isepe kumbe wanajidanganya wao...eti mungu katuepusha , uongo mtupu

Kama kuna tambiko limefanyika na watu hawafi shida iko wapi bwashee.
 
Kama Korona imeisha huwezi kuitumia korona kama kisingizio cha kusitisha mkopo, Watafute kisingizio kingine chenye mashiko.

Watu mtaani hata barakoa hawavai tena, sasa hiyo korona ya excuse ya kuombea usitishiwe mkopo iko wapi?

Narudia korona hata kama imeisha bado uchumi umeathilika sana hata huko ulaya taasisi za fedha zinatoa pesa kwa ajili ya ku busti uchumi zao kwani tayari zimeathilika,
Sasa itakuwaje tanzania tusihitajibunafuu?
Makusanyo ya kodi yamepungua wakati mahitaji yanaongezeka sasa hizo pesa hazihitajiki kivipi mangi?
 
Hilo la uchumi wa nchi yetu kuyumba na makusanyo ya kodi kupungua umeyapata kwenye ripoti ipi? au unahisi tu?
Kama yamepungua, yamepungua kwa sh ngapi?. No data no right to speak
 
Sisi uchumi umeathirikaje wakati corona ilikaa wiki 2 ikaisha kwa maombi?
 
Data za serikali zinaonyesha uchumi unakua kwa kasi haujaathirika na chochote. Corona ilikaa wiki 2 ikaisha kwa maombi. Uchumi gani umeathirika?
 
Mbona siye tushaimaliza hiyo corona
June 10 bodi ya wakurugenzi wa shirka la fedha Duniani na Bank ya Dunia kuamua iwapo tunastahili kupewa msamaha na mkopo kupambana na corona au laa.

Mwezi April IMF na WB walitengeneza kitu kinaitwa Catastrophe Containment and Relief Trust ili kusaidia nchi masikini kupambana na madhara ya corona.

Kwenye hiyo relief programme nchi masikini zitasamehewa kulipa madeni yake hadi miaka 2.

Tanzania tumeomba tusamehewe chini ya hiyo relief programme ili tupate pesa ya kutusaidia kupata vifaa tiba vya kupambana na corona.

Kwenye barua yake ya kuomba serikali imesema imeshindwa kufanya vipimo na kufuatilia muenendo wa corona kwa sababu ya ukosefu wa pesa.

IMF imesema June 10, 2020 bodi itaamua kama tunakidhi vigezo kusamehewa au lah.

Soma barua ya IMF kwa serikali.View attachment 1469742

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
utashangaa wanatoa mkopo na deni la nyuma wasameh[emoji23][emoji23].

yaani mabeberu huwa wanawaza kuwakomoa CHADEMA tu,hamna kingine.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Sisi uchumi umeathirikaje wakati corona ilikaa wiki 2 ikaisha kwa maombi?

We bado mvulana kwa hiyo huwezi juwa, na kwa kuwa unakula bure ni haki yako useme hivyo.
Mpaka sasa kuna watu hawasafiri kibiashara kununua mizigo nchi zingine, watalii hawaji kwa kiwango, ndege hazitui wala kuruka madisco na masherehe hayapo, wewe hata hilo huoni tu au ujinga ndo mzigo uliobeba.
 
Wewe na rais nani anajua zaidi? Mimi namikiliza rais wangu anasema corona iliisha baada ya maombi na uchumi unakua kwa kasi. Haya mengine wewe umeyatoa wapi?

Mimi kua mvulana au kutokua, au kula bure kunahusiana nini na kauli ya rais wa nchi?

Unataka niamini maelezo yako wewe mvimba macho kuliko kauli ya rais? Hivi unaakili kweli?
 
Siwezi kukujibu tena mtu unayetegemea chenji za mboga,
Usipotumia akiri zako utabaki kushikiwa kila siku,
Baki.na ujinga wako maana umeamua kuwa hivyo.
Achana na sisi tunaowatafutia chakula ili mule ndo tunajua nini kinaendelea.
 
We bado mvulana kwa hiyo huwezi juwa, na kwa kuwa unakula bure ni haki yako useme hivyo.
Mpaka sasa kuna watu hawasafiri kibiashara kununua mizigo nchi zingine, watalii hawaji kwa kiwango, ndege hazitui wala kuruka madisco na masherehe hayapo, wewe hata hilo huoni tu au ujinga ndo mzigo uliobeba.
Tumeambiwa watalii wameanza kumiminika au Kigwangala muongo.
 
Back
Top Bottom