Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

Katika maisha yangu ya kutazama soka, sijawahi kuona mtu anapiga freekicks kama huyu mwamba, najua wapo kina beckham, ronadinho, messi, zidane, fundi pirlo, cr7, shunshuke nakamura na wengine wengi, ila juninho hana mpinzani, jamaa alikuwa hatar, zaidi ya hatari, kwanza hakuwa na eneo maaluum tofauti na hawa wengi ambao kuna sehemu na sehemu, jamaa ilikuwa popote anakuweka..

Inakadiriwa alifunga magoli ya freekicks yapatayo 80 kasoro kidogo katika official matches.. jamaa alikipa sana lyon ile iliyobeba ubingwa mara 7 mfululizo, katika goli 100 alizofunga pale lyon basi 44 ni za faulo..
Na upigaji wake ndio kuna baadhi ya wachezaji wamechukua kwake..

Heshima kwako juninho pernambucano.
Mkuu umesahau watu wawili
Gheogre Hagi na Hirsto stoichkov
 
Sio lazima kila mchezaji nyota acheze hizo timu! Unamkumbuka All time goal scorer wa EPL? Unajua aliwika wapi na alistaafia wapi? Unamfahamu mtu alieitwa DEVOR SUKER? Hao waliwika pasi na kuchezea hizo timu ulizotaja!
Kwa nyakati tofauti suker alikipiga madrid na arsenal.. Nakumbuka kuna game na liver alituchomesha alikosa penati dk za nyongeza kabisa. Nadhani ni msimu ambao titi camara alikuwepo liverpool
 
Piere van hoojdoonk ktk game moja hiv siikumbuki alipiga faulo ya kwanza ikagonga besela... Ikatokea mistake hiyo faulo ikarudiwa akapiga tena ikagonga pale pale ilipogonga besela faulo ya kwanza
Kuna jamaa nmemsahau aliwahi kutia hat trick ya freekick.
 
Ile ndio ilikuwa brazil haswa.
Timu ya taifa ya brazil kwa miaka hiyo zilicheza kitimu sana badala ya kutegemea uwezo wa mchezaji mmojammoja.

Mchezaji alichaguliwa kwa jinsi anavyosaidia uchezaji wa timu. Ndo maana watu kama elber hawakuitwa japo walikuwa wanawika sana ulaya.
 
Katika freekick na corner bado sijaona wa kumzidi JUAN ROMAN REQUELME huyu ni mwa Argentina alikuwa ni balaa enzi zake alikuwa anajua anachokifanya,, tunamuona Messi nae kafuata nyayo zake.
 
Back
Top Bottom