Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

Juninho Pernambucano: Mpiga freekick bora kuwahi kumtizama

Bangi ukiitafuna ina madhara sana yani akina Casillas, Buffon, Petr Cech, Dida nk uwaite makipa uchwara ina maana hawa akina Oblack, De Gea, Kepa, ndio bora? Kuweni na adabu japo kidogo

Mahaba yamekuzidi,,,punguza jombaa

Unawajua hawa👇🏿au ulikuwa bado unanyonya

Messi
Beckham
Requelme
 
Mahaba yamekuzidi,,,punguza jombaa

Unawajua hawa👇🏿au ulikuwa bado unanyonya

Messi
Beckham
Requelme
Hao akina Beckham na Riquelme usiwaoredheshe sababu walikuwa katika zama za Juninho (Kipindi ambacho wewe unadai kilikuwa na makipa uchwara) Kuhusu huyo Messi ana goli ngapi za Freekick ? Goli lake la mbali zaidi la Freekick lilikuwa na umbali gani?
 
Benzema mtoto mdogo tuu kwenye Ile Lyon...mbele kulikuwa na sonny Anderson,Sydney govou, wiltord,malouda..baadae akaongezeka elber..kiungo ndio balaa..pernambucano,vikash dhorasoo,mamadou diara,essien,edmilison..mabeki cacapa,cris,liverile,pasquale..huku golin yupo coupet..manager Claude le puen..
Huyo mtu wakuitwa vikash Dhorasoo alikua anahatari bonge moja la play maker halafu alikua na uwezo mkubwa wakutembea na mali best dribler. Dah na hilo beki lao Cris lilikua linakula upara masaa yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kufananisha vitu vya kipumbavu na mtu kama pirlo, ronadinho,beckam

Free kick ya beckam ilikua inatumika kufundishia physics huko ulaya kwenye topic za projectile motion.

Who is juninho? Brazil hata hawamjui.

Katika maisha yangu ya kutazama soka, sijawahi kuona mtu anapiga freekicks kama huyu mwamba, najua wapo kina beckham, ronadinho, messi, zidane, fundi pirlo, cr7, shunshuke nakamura na wengine wengi, ila juninho hana mpinzani, jamaa alikuwa hatar, zaidi ya hatari, kwanza hakuwa na eneo maaluum tofauti na hawa wengi ambao kuna sehemu na sehemu, jamaa ilikuwa popote anakuweka..

Inakadiriwa alifunga magoli ya freekicks yapatayo 80 kasoro kidogo katika official matches.. jamaa alikipa sana lyon ile iliyobeba ubingwa mara 7 mfululizo, katika goli 100 alizofunga pale lyon basi 44 ni za faulo..
Na upigaji wake ndio kuna baadhi ya wachezaji wamechukua kwake..

Heshima kwako juninho pernambucano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utasemaje master wa eneo moja,wakati timu ikiwa imezidiwa au kuwa nyuma kwa goal/goals wachezaji wenzake wanajitahidi kutafuta faulo popote karibu na lango la wapinzani na ikitokea anawaweka?hiyo ndio Plan B.

Sent using Jamii Forums mobile app

Plan B na plan A ipi inaanza? Ukijua hilo utakua umepata jibu.
 
Utakuwa na makengeza wewe.

Nyuma ya mafanikio ya Olympic Lyon ya 7 years consecutive titles alikuwa Juninho Penambucano.

Lyon hawa walimtoa Real Madrid kwa miaka mitatu mfululizo kwenye UEFA champions League quarterfinals.

Juninho ndiye alikuwa fundi wa pale central midfield akitawanya mipira kama hana akili timamu.

Unazungumzia timu kubwa kutomhitaji ? Mbona Allan Shearer hakuwahi kuhitajiwa na hizo timu za Real Madrid unazozitaja hapa.?

Sent using Jamii Forums mobile app

Walimtoa RM afu wakaishia wapi?

Unaweza kumtoa mtu sio sababu ya uwezo wako bali sababu ya udhaifu wake.

Unaongelea league1, farmers league, one-sided league. Ile ni league dhaifu kuliko zote in Europe's top-flight leagues.
 
Greatest Free-Kick Takers of All Time.
kwa mujibu wa daemusin kwa msaada wa youtube.
  1. Juninho pernambucano
  2. Sinisa Mihajlovic. (mtafuteni huyu jamaaa kwa ambaye hajamuona)
  3. David beckham
  4. ronald koeman (anafundisha uholanzi)
  5. lionel messi
  6. Gheorghe Hagi na wenzake waliobakia
 
Acha kufananisha vitu vya kipumbavu na mtu kama pirlo, ronadinho,beckam

Free kick ya beckam ilikua inatumika kufundishia physics huko ulaya kwenye topic za projectile motion.

Who is juninho? Brazil hata hawamjui.



Sent using Jamii Forums mobile app

Ama kweli we tabutupu!! [emoji13][emoji13][emoji23]🤣

Sasa brazil wasimjue juninho kacheza wordcup mbili!

Halafu tofauti ya juninho na wapiga freekicks wengine wengi! Jamaa hakuwa na sehemu maalum wala umbali! Yeye iwe kushoto, kulia mita 35 sijui huko anakutungua! Alishawahi kuwatungua barcelona goli freekick karibia na sehemu ya kona!

Halafu mzee kwenye projectile motion hapo unatupiga changa la macho! Unaijua projectile motion vizuri mzee kama ni faulo zilizokuwa zinakwenda kiprojectile motion basi za juninho ndio zina hadhi hiyo! Mpira unapigwa unapaa juu ya ukuta kisha unashuka chini kwa kipa unadundia chini hiyo ndio projectile motion
Sio hawa wanapitisha juu ya ukuta unaenda kuingia kwenye kona ya golikipa huko unathubutu vipi kuiita hiyo ni projectile motion!
Hebu tupe definition ya projectile motion na michoro miwili mi3

Halafu nipe link kuwa faulo za beckham zilifundishiwa projectile motion!



Nb: sisemi kuwa beckham alikuwa mpigaji faulo mbovu la hasha alikuwa mzuri tena saana ila kwa juninho anasubiri hata rekodi zinatuonesha, pili hapo kwenye projectile motion hapo unipe ushahidi ndugu yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimtoa RM afu wakaishia wapi?

Unaweza kumtoa mtu sio sababu ya uwezo wako bali sababu ya udhaifu wake.

Unaongelea league1, farmers league, one-sided league. Ile ni league dhaifu kuliko zote in Europe's top-flight leagues.

Mada haizungumzii juninho ni mchezaji bora kuwahi kutokea, mada ni juninho mpigaji freekick bora kuwahi kutokea.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom