Boss, hii mada hutapata wanawake wengi wana admit ukweli.Si unajua tena wanawake kwa pretences hutuwezi! lol
Hivi mnadhani kwanini dini nyingine zinaweka mipaka baina ya wanawake na wanaume? Mvuto wa asili uliowekwa na muumba kuukabili yataka nguvu ya ziada.Angalia watoto wanapozaliwa hadi wanafikia umri wa kujitambua, utaona "pairing tendencies" na hata utaona ishara fulani fulani kuashiria "mvuto"huu! Najua wanawake wenzangu wengi hujaribu kudanganya ati hakuna kitu au ati ni rahisi urafiki baina ya ke na me bila "mvuto". Nimeona na kushuhudia marafiki wa namna hii, mmoja anapata mvuto wakati mwingine havutiwi na kwa sababu ya kulinda urafiki, yule aliyevutiwa hujikausha kisabuni.Wakati mwingine yule asiyevutiwa, hujua kuwa mwenzie anamzimia, ila kwa vile yeye hana mpango huo, hujifanya hajaona na kwa vile kuna "benefits" fulani hupata na siyo lazima material benefits - hata ile kampani tu, basi urafiki huendelea.