Just a friend na matatizo yake.....

Just a friend na matatizo yake.....

Sisemi kama ni rahisi, hasa kwa wale wenye akili ambazo haziwazi chengine zaid ya ngono, lakini inawezekana sana kwa wale wanaowekeza katika urafiki. Kitu cha muhimu ni kwa "victim" ambao mara nyingi huwa ni wasichana, kuwa na msimamo tangu mwanzo anataka nini na kuwa muwazi. Iwapo mmoja atakuwa na hisia tafauti na mwengine kiasi cha kuonesha kwa ishara, maneno au vitendo, lakini mwenzake akaweka mipaka tangu mwanzo, hapo ndipo palipo na mtihani wa kujua kama kweli alikuwa anakutaka "just as a friend" au alikuwa anakutaka kivyake.
Baada ya kumwambia wazi, "na mimi ninakupenda lakini kama rafiki", anaweza kukata "urafiki" hapo hapo, akaendelea kumwaga sera au kubakia kama rafiki na kukuheshimu.

Pia kama walivyosema wengine, urafiki wenu unaweza kuendelea mpaka pale mmoja kati yenu atakapofunga ndoa. Ikiwa mume/mke wa rafiki yako ni katika wale wachache wanaoamini kuwa urafiki baina ya jinsi mbili unawezekana, mtaendelea kuwa marafiki kwa yeye kuwa rafiki yenu, lakinimmoja wenu akisema "the festival is over" hakuna cha urafiki, basi utaishia hapo.
 
Uzoefu wangu ni kuwa...Inawezekana kutegemeana na ukaribu ambao upo baina yenu,ni nini mnazungumza na uwazi uliopo baina yenu....na kama kuna commitment fulani ambazo mmoja wenu anazo ambazo upande wa pili lazima aziheshimu....kuumia inawezekana kwa kweli,mfano best friend wako kaoa na unafurahia jinsi anavyomtunza mke wake,lazima ka wivu katakuwepo hata kama hakuna kitakachoendelea baada ya huo wivu....yamekushinda naona The Boss....lol
Kama ulivo sema hapo juu, kudevelop hisia kwa rafiki yako sio kosa, na in fact it doesn't change the friendship. Ni what you do with the feeling that will. Kama nitaweza kumeza feelings zangu na kuzisuppress kabisa before they escalate to love basi hakuna ubaya... And I expect the same from him.
It is a bit more complicated kama kuna watu wengine involved, mfano wahusika wana wapenzi etc.
 
Hahahaha wivu mbona hata wanaume wanao bana?
Alafu ukiwa na wivu na mtu jichunguze. . .
Nna rafiki yangu nilifahamiana nae akiwa single na recently kapata mtu wala hainiumi, nafurahi nikisikia anafurahia mahusiano yake na yasipoenda vizuri ntasikitika nae.
Niliandaa harusi ya rafiki yangu saanaaa.......... nilifurahia sana alipopata mwenza. na mpaka sasa yule wife anajua hawa bwana siwawezi, anaishia kusema niwaache tu maana niliwakuta hivyo hivyo, sitawatendea haki nikiwaachanisha
 
Niliandaa harusi ya rafiki yangu saanaaa.......... nilifurahia sana alipopata mwenza. na mpaka sasa yule wife anajua hawa bwana siwawezi, anaishia kusema niwaache tu maana niliwakuta hivyo hivyo, sitawatendea haki nikiwaachanisha
Jamani soo sweet.
Nyie wote wanne mmebahatika kukutana wote waelewa.
I love it!!
 
some friends are very hard to find
hutaki kuwapoteza kabisa
sema hata kama ni rafiki wa kiasi gani
lazima uoneshe msimamo wako
kama wa hapana weka clear boundary
kama wa ndio haya napo twende kazi
nakubaliana nawe 100%, siyo swala la kukataliana na kuvunja urafiki just like that, unafanya cost benefit analysis ndo unafanya maamuzi. watu huwa ni waelewa sana, hasa kama ni marafiki wa kweli. kuna siku tuliwahi kulijadili hili swala na rafiki yangu na tukakubaliana kabisa kwamba hatutapungukiwa kitu kama hatutaenda next step kwenye urafiki wetu. kweli kila mtu alikuwa na feelings na mwenzake baada ya muda lakini kila mtu alikuwa married, kwa hiyo hakuna future kwa ambalo tungelianzisha. mpaka sasa tupo bomba tu
 
My best friend ni mkaka, yaani huyu tumesoma wote, namwambiaga vitu vingi nayeye pia..plus mambo mengine ya maisha..hamna baya lililotokea..birthdays atanipa zawadi mie pia nampa hata tuwe mbali vipi...ana relationship ya muda kweli na mimi pia nadate..kila mtu anamfahamu shemeji wa mwenzie!
 
My best friend ni mkaka, yaani huyu tumesoma wote, namwambiaga vitu vingi nayeye pia..plus mambo mengine ya maisha..hamna baya lililotokea..birthdays atanipa zawadi mie pia nampa hata tuwe mbali vipi...ana relationship ya muda kweli na mimi pia nadate..kila mtu anamfahamu shemeji wa mwenzie!

Jaribu siku moja kumwambia unataka ulale naye uone atasemaje...
 
Inawezekana kabisa Boss, kuwa na urafiki na mtu wa jinsi tofauti wala msiwe na mawazo ya kingono,
 
Inawezekana bana Boss mbona mie na wewe ni marafiki wa kawaida?au unaumia chini chini hujawahi niambia?

Nina marafiki wengi wa kiume lakini kuna wawili ambao wamekuwa kama sehemu yangu ya maisha. nilisoma nao kuanzia high school mpaka chuo na hata hostel tulikaa moja. na nawapenda kwa udhati kabisa. wakati wa tabu na raha tuko wote na sijawahi kuumia kichini kichini. na naamini pia wao hawaumii kichini chini.so its possible if you put your mind into it.
 
kwa sababu viungo vinafanya kazi
na mnaitikia vichocheo

tena kama mmekula na kushiba ndo hala hala
dont try that hotelini

pia mkiwa below 26 mnaweza
sababu vichwa vinakuwa na tamthilia 90%

sasa nina miaka 42
nimnyime mwenzangu nini?
Hata asipotumia yeye
kuna mwingine atatumia tu

kuna msemo huu
'majirani hawafichani makalio'
si ndo mnaosaidiana wakati wa shida na raha!

...hapana bana...nilijifunza mental discipline miaka ile ya unjuka boarding school...

Enzi hizo Disco za wanafunzi DJ anaunganisha blues zote za Lionel Richie kuanzia
stuck on you, hello, 3times a lady, kisha time after time ya Cyndi Lauper kabla hajamalizia na
Sexual healing ya Marvin Gaye..- kizani!

kufumba na kufumbua ukumbini taa zinawashwa halafu DJ anaweka Oye co Mova...-Santana.
Kwakuwa niliijua routine, haikuwa taabu ku switch off akili kabla ya kuadhirika na suruali zangu
za mchele mchele miaka hiyo...

Huku ukubwani it's the same...na switch off tu mawazo ya ushwetani, hata kama na share kitanda!
 
"Just a friend" ni kalugha ka kufichia hisia za mahaba kati ya watu ambao bado hawajaweza kufafanua mvuto wa kihisia uliopo kati yao!
 
Back
Top Bottom