Juventus Special Thread

kama nilivyosema huyu mtu ni muhimu sana ALEX SANDRO jana kaingia tukacheza 4-5-1 na kusema kweli tulikuwa tushajiandaa na draw, pogba akaingia kati alafu sadro akacheza pembeni, mpira wake alio urudisha kwa kichwa usitoke ndo ulizaa goli,

lakini Lucky played a part, pia great turn kwa MTUKUTU SIMONE ZAZA, kumgeuza gholubary na kupiga strike ile

FORZA JUVEEEEE,, waitin for bayern GOD BE ON OUR SIDE
maana injury zimetuandama mungu saidia RUGANI dogo akomae na kina MULLER, kam jana alivyokoma na kina gonzalo
 
Sweetheart nilikua porini, mufindi ndanindani huko, game niliona second half mjini Iringa pale wanapaita Club VIP na nadhani club yote buluda nilikua man alone, ila wote walitambua uwepo wangu baada ya ule mkwaju wa Zaza, na tena nilikua counter, hakika vijana walinifurahisha though injury ya Kiongozi Bonucci ilinifikirisha sana

Pole Mamy, naona big Sam aliwaongezea maumivu, Mzee wa philosophy hamumtupii virago tu? Mje Italia mpate kocha bora, yupo Conte na atawafaa sana
 
Mzee tunawahitaji Bonucci na Chielini ASAP, hata mmoja wao tu kukabana na kina Lewa ndoo ya whiskey, na Zaza aanzishwe hiyo game alongside Dybala, Moratta kaanza uvulana wake, arudi bench kidogo

Sandro mtamu sana kwenye mashabulizi, lakini bila ya Bonucci na Chielini tutahitaji uzoefu wa Evra kukabiliana na mkoloni
 
Pole na safari dear kimya kimya hatuagani au ndo ulichepuka kidogo...lol

Mkwaju ule ulikuwa balaaa......hope mtawapiga Bayern,Chiellin Muhimu sana kuwepo.

Sweet acha tu LVG ataniua mwisho usinifaidi bure!!,tumebaki jina tu,Mpira hakuna anyway ngoja tuendelee kusubiri maana Naona Woodward anamkingia kifua LVG.
 
Miezi dume hii Mamy, shilingi inatafutwa mpaka porini. Sijawahi wala sina mpango wa kuchepuka, radha zoote unazo sweetheart from bedroom to the kitchen, I can only be greatful [emoji120]

Huyo mkoloni ananipa kihemuhemu kwa kweli na yale majeruhi ya beki yangu, ngoja nitafute updates za Bonucci labla kuna muujiza umetokea siku ya wapendanao

Mjiangalie msigeuke AC Milan ya England, maana hata Champions League msimu ujao kuna hatari mkaungana na Liverpool kwenye mashindano ya alhamis
 
Mkuu wakti umetaradadi, mkoloni yupo mlangoni. Tutete kidogo tactics zitakazotupa ushindi usiku wa leo

[HASHTAG]#BeHeroes[/HASHTAG] [HASHTAG]#FinoAllaFine[/HASHTAG] [HASHTAG]#ForzaJuve[/HASHTAG]
 
Forza Juve !!! Forza Juve !!!........

Mpoooooooo???? Mbona kimyaaaa? Juve piga huyo mjerumani.....
 
Naona kwa mara ya kwanza Arturo Vidal karudi Turin tangu alipoondoka transfer summer iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…