mkuu we ndo kiranja hapa kwenye huu uzi, inabidi uwe unaweka hata tetesi zozote zinazohusu timu yenu. Hata hivyo wadau wa serie a wamepungua sana. Kwa sasa watu wapo kule kwenye epl.
Ahsante kwa hunipa changamoto, juve2012 anasema mapenzi yatarudi mpaka tukipata mafanikio ulaya, Viper sijui mujiri wake, bologna naye sijui yuko kwenge palizi na hawa wadau wengine sijui niwaPM? eti nisaidie Pweza Pazi, Chimunguru, Mlaleo, myao wa tunduru, karibuni tena jamvini
juventus bado ni moja ya club kubwa barani ulaya. Lakini kama kina juve2012 wamepunguza mapenzi na clab yao, eti haina mafanikio ulaya, itawabidi wasubiri kweli.
Juve kufikia level ya Bayern Munich, Real Madrid, Barcelona na Man city itawachua muda. juve2012 unafanya makosa kukimbia timu yako, usiwe kama Ngongo japokuwa wewe hujaama.
juventus bado ni moja ya club kubwa barani ulaya. Lakini kama kina juve2012 wamepunguza mapenzi na clab yao, eti haina mafanikio ulaya, itawabidi wasubiri kweli.
Juve kufikia level ya Bayern Munich, Real Madrid, Barcelona na Man city itawachua muda. juve2012 unafanya makosa kukimbia timu yako, usiwe kama Ngongo japokuwa wewe hujaama.
juve2012 naona Mkuu umeandika kwa uchungu wote, pole sana
Ila tukiangalia on the positive side of it, Bianconeri inaelekea pazuri ingawa sio pazuri sana lakini tunaweza kusema at least kwa sasa club iko stable, na stability ndio kitu kikubwa na cha kwanza katika kujenga mafanikio
Tuko stable na kocha, kikosi chetu (tetesi za leo zinasema Vidal anakaribia kusaini mkataba mpya wa thamani ya £200k kwa week) na pamoja na ufinyu wa budget ya club tunajaribu kutafuta wachezaji kuimatisha kikosi, kina Osvaldo, Tevez, Llorente
Yaliyopita si ndwele, lets play our party na ninaona kabisa Juventus ikitia jitihada za dhati kurudisha heshima na hadhi yake barani ulaya.
Forza Bianconeri
amen mkuu,ahsante kwa moyo wako wa kutokukata tamaa,unatutia moyo na wengine wenye mioyo fragile.Unajua mtu ukipenda sana ni rahisi kukata tamaa ukiudhiwa.Mimi naumia kwa vile naamini matatizo ya Juve ni ya hujuma za watu wengine na wametuumiza sana ila kama ulivyosema mkuu,huu ukoo wa Agnelli uko stable sana.Tumeshuhudia klabu kubwa zikiuzwa lakini Agnelli pamoja na majanga yote yaliyowakuta(kushuka daraja,uchumi wa Italia kuyumba,kufariki Umberto Agnelli,kusuasua kwa soko la Ferrari ulaya,kusambaratishwa kwa ukoo wa Ghadaffi waliokuwa wamewekeza sana Juve,kuondoka kwa Juve kwenye soko la hisa,kufa kwa serie a n.k) wametulia na Juve yao,wamebalance vitabu vya hesabu,wamekuwa patient,wameintergrate uwezo wa kifedha na kiufundi kuinyanyua timu wakitoka kuunda kikosi chenye average players wengi walioiweka Juve kuwa timu nzuri italia hadi sasa wanahama toka timu nzuri hadi nzuri zaidi kwa kuchanganya average players na quality players na muda si mrefu watajaza champions na kuwa timu bora.Cha msingi ni kuhakikisha mipango yao inazaa matunda uwanjani.Ndio maana nataka sana mafanikio ulaya,si lazima kutwaa kombe bali kufika robo au nusu fainali mara kwa mara kutawapa fedha nzuri kumanage wachezaji bora,technically watajenga base nzuri ya uzoefu wa kuendelea kutesa Italia na kuwa wakali wa ulaya baadae.Hii mizengwe ya Italia inanifanya nipendelee Juve kutupia jicho ulaya kwani zipo timu(kama Basel ya uswisi,za urusi na ufaransa)ambazo pamoja na kutokea ligi dhaifu kuliko serie a bado zimeweza kujiestablish as a force ulaya.hata Munich ilifanya hivyo wakati ule bundesliga ikiwa hoi na bado wakawa tishio na leo hii ligi imekuwa bora Bayern wamefaidika mara mbili.
Hofu yangu kubwa iko kwa A.C Milan!wenye timu wako shaghalabaghala kila mtu na maamuzi yake!Berlusconi nae politiki zinamchosha akili.Wamuachie timu uncle Festa watafanya la maana.Milan inapaswa kuundergo revolution kama ya Juve wakati ule walipouza robo tatu ya timu,wakanunua wachezaji wapya,wakabadili makocha hadi kumpata Conte,wakabadili directors hadi rais wa timu!Pale Milan uncle Festa anastahili kukabidhiwa nafasi yenye maamuzi makubwa sasa.Yule jamaa analijua soka na fitna zake.
Tutafika tu hata kama itatake time lakini msimu huu tukomae na Europa na hii scudeto, pesa zitakazopatikana hapa zitaweza kutusaidia kuongeza depth and quality ti our squad
naam,kabisa mkuu Mourinho.Muacheni tu Gang Chomba mzee wa watu ajipumzikie,hizi frustrations za serie a zimetuliza wengi.Naona kaka mkubwa naye kimyaa,maskini!usijali Chomba tutarudi tu siku moja kwenye level zetu.
Hahahahaaa, kaka mkubwa yupi mzee?
Mkuu ilikuwaje Verona wakarudisha goli dk za majeruhi?ule ndio upuuzi nisioutaka pale Juve.
ina maana humjui kweli kaka mkubwa wetu wa haya majamvi ya kirumi au unataka nimtaje ilimradi tu upate mahali pa kuanzia vijembe vyako ?si nimeshamtaja hapo juu?a.k.a uncle festa teh teh!
Mara ya mwisho alionekana JF doctor jpili iliyopita anaomba ushauri kutokana na tatizo la akili kushindwa kudhibiti mawazo.Akasema kuwa wenye nafasi nzuri ya kumshauri kutokana na experience waliyonayo ni mashabiki wa Man U!
Mara ya mwisho alionekana JF doctor jpili iliyopita anaomba ushauri kutokana na tatizo la akili kushindwa kudhibiti mawazo.Akasema kuwa wenye nafasi nzuri ya kumshauri kutokana na experience waliyonayo ni mashabiki wa Man U!