hakika Shifta alifikisha salam za pongezi kwenu ndugu zangu...
nami kwa uungwana zaidi nawapa tena pongezi
Mkuu kwa haraka haraka unaweza ukasema umeshaingia nusu fainal....lkn kwa mtazamo wangu hizi timu za Ufaransa sio za kubeza hata kidogo. hasa hawa Monaco ingawa unaweza sema PSG ni wazuri kuliko Monaco lkn mashindano ya UEFa ni magumu sn na timu zinajiandaa sn....ngoja tuone ingawa waitali nao wana sifa zao babkubwa ktk hatua za mitaona km hii.
Hongereni sana..
Mzee mwenzangu nilikua safari kidogo, huyu pweza huyuu! Hahahahahahahahaaa, Uefa hii inaweza kuwashangaza baadhi ya vigogo, ile combo ya Carlitos na Morata hakuna beki inataka kukutana nayo
#FinoAllaFine #ForzaJuve #Juventino
yah,pole mkuu.Ile kombinenga ni misumari ya inchi 6,ukikanyaga inatoboa hadi rim teh teh!
Usiifananishe PSG na Monaco, wakati PSG wameendelea kuimarika hasa psychologically hawa Monaco wamekua weakened kwa kawapoteza wachezaji wao wawili muhimu, Rodrigez na Falcao na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara hasa kwa maveterani kama Cavalho na Tulalan
Hebu angalia kikosi cha PSG halafu niambie team ngapi Ulaya zinaweza kuimatch PSG kwa individual talent and squad depth, can the same be said about Monaco? Akiumia Moutinho, nani mbadala wake? Ingawa nyie Chelsea mlitolewa kwa uzembe wenu wenyewe.
Juventus sio Arsenal Mkuu, mawazo yetu yapo kwenye semis
kweli kaka,ngoma bado hii!hii ni robo fainali na kila timu iliyofika hapo haijafika kwa kucheza mdundiko,bali mpira uwanjani.nilikuwa natania tu,ila naona ni heri tungepewa timu kubwa kama Real ili morali iwe juu kuliko hizi timu zisizoeleweka,huwa ni ngumu.Juve wanatakiwa kufuata ushauri wa Tevez,kwamba Monaco ni the worst draw, bora wangepewa Real au Barca.
Kuna haja ya kuanza kumanage kikosi chetu kwa kuangalia zaidi Ulaya kuliko nyumbani, kina Tevez, Marchisio, Vidal, Bonucci wanahitaji kupumzika kidogo kidogo na mmoja mmoja bila kuharibu balance ya team
Nimekusoma hapo juu ukiakisi mawazo ya Carlitos, ni kweli Monaco wanaweza kuwa wasumbufu kwa sababu they've got nothing to lose, lakini bado naona ni bora mara 100 kukutana na Monaco kuliko Barca, Bayern katika stage hii, ngoja tuwabalase hawa ili confidence ikue ndani ya kina Morata then waleteni wowote wale tuwachezeshe kwata la kibuluda.
#FinoAllaFine
#ForzaLaVecchiaSignora
#ForzaJuve
#ForzaBianconeri
santee!pole na mbilinge za Hull city!
Mkuu ata mimi nimesema hapo juu kua PSG ni wazuri kuliko Monaco. rudi ukasome post yangu tena uone mkuu....
Ulichosema ni kweli mkuu ata mimi nimehofia sn huo mchezo wenu na kuona kua morari yenu itashuka.
Jana mlishinda kwa taabu sn lkn nafikiri hili ni kutokana baadhi ya wachezaji wenu kuanza kuchoka.....
Aisee mambo yalikua magumu jana kaka....
Umeanza mambo ya yule Bauncer waliomnanii kichakani kwa mbindee sana, ungekua unajua historia ya hivyo vijamaa ungemuelewa juve2012 alivyofurahia ule ushindi.
So far hatuna wachezaji wenye uchovu but Allegri needs to manage the squad well kama tunataka kwenda mbali zaidi kwenye UCL, kina Vidal, Marchisio, Pereyra, Morata na Tevez ni kama ndio wanaanza msimu, they're on fire, kina Barzagli ndio wamerudi kutoka kwenye majeruhi, bado kina Asamoah wapo njiani, so far hatuna tatizo la fatigue Mkuu
Team yako ndio inaumwa uchovu na kocha wenu alivyo king'ang'anizi hataki kabisa kufanya mabadiliko.
Ivanovic, Terry, Matic, Willian wanahitaji kupumzishwa or else mna hatari ya kupoteza points kwenye game zilizobaki maana kila match mtakayocheza itakua ni fainali, kila team itawakazia
Mkuu kwa sasa tunacheza EPL tu mara moja kwa wiki...wachezaji watachoka vipi hapa mkuu?
Matokeo ya jana mkuu ni makosa ya wachezaji wenyewe na si uchovu mkuu....
Ni kweli kuna hatari ya kudondosha point mkuu hasa kutokana na timu kuikania sn chelsea lkn mimi mashaka yangu makubwa ni kufanya fitina mkuu kwa waamuzi.....lkn kutona na ratiba ilivo ya timu zote bado tutakua hapo hapo juu...na uzuri wajina lako Mou ligi ikiwa ktk muda huu na anaongoza basi kumtoa juu inakua ni shida sn....
Mkuu uchovu sio wa team kucheza kila baada ya siku 3 na kuwa na muda mdogo wa kupumzika, ni accumulation ya uchovu toka mwanzoni mwa msimu, we hujiulizi kwanini siku hizi hamtandazi lile soka mlikua mnapiga kabla ya mwaka kugeuka?
Hivi kuna winga au mchezaji alikua anampita kirahisi Ivanovic kama jana au kwenye ile match na Spurs mliyopigwa 5? Fabregas alikua anaweza kukaa muda wote huo bila kutengeneza goal? Matic alikua, ulipo mpira na yeye yupo, yeye na Fabregas walikua wanacover sehemu kubwa ya uwanja kuliko mchezaji yeyote kwenye ligi, siku hizi je?
Bahati yenu ni kuwa kiwango cha ligi yenu msimu huu ni cha hovyo sana ndio maana bado mpo kileleni, or else tungekua tunaongea mengine saa hizi, kule La Liga Madrid walianza kama nyie ila walivyodrop tu Barca haooo
Ninakubali mkuu kua kuna kushuka kwa viwango kwa wachezaji na ndio maana tunaona kuna makosa yanajitokeza sn wakati mwingine....lkn pia nimeona kua Chelsea wana kikosi kidogo sn ndio maana timu ni hiyo hiyo moja inayoanza siku zote.........lkn bado wanafanya vzr pamoja na changamoto zote hizo.....
Ngoja tuone msimu ujao mambo yatakavokua......
Khaaaa, Ntuzu huna haya? Chelsea mna kikosi kidogo?
Ukiacha Man City sijui ni club gani ina depth kwenye squad kama Chelsea hapo EPL
luciano Moggi bado anabwabwaja tu kuhusu Calciopoli