Naona Allegri anafaulu mtihani ambao ulimshinda Conte,combination ya Pogba +Tevez + Morata imewabeba sana.Kwenye Serie A ubingwa uko mkononi na Champions League almost mko nusu fainali.Natamani sana mchukue ubingwa msimu huu
Hii ngumu kumesa sasa, alianza Pirlo, akaja Pogba sasa Marchisio tena for the rest of the season, kichwa kinaanza kuuma au juve2012 utakamata dimba mzee?
mkuu acha tu.leo tumecheza ovyo pale kati tumepoteza mipira vibaya.yaani ni disaster.kama Empoli wametusumbua vile,hiyo Monaco itakuwaje?
Umenena vyema mkuu. Game ya Jana kwa akili ya kawaida niliiona ngumu sana. Kwanza juve clinic yao imejaa majeruhi, pili viola walikuwa nyumbani nilitegemea mpambano uwe mgumu. Cha kushangaza First half mlikuwa tayari mpo mbele kwa goal 3. Kuhusu kukutana na Napoli hilo halikwepeki. Leo Lazio anaondoka hili halina mjadala...Alegri kaiweza juve akifanikiwa kuiondoa Monaco basi msishangae akachukua ndoo kabisa.
Ntuzu huwa unaangalia game za Juventus au wewe ni EPL tu Mkuu? Nasikia mnamtaka sana Pogba, tupeni Oscar na pesa tuwape the Pogboom
Tuna kijana anaitwa Pereyra, umemuona huyo?
Najua kwa sasa hatupo kwenye kiwango chetu, pamoja na hayo Lazio hawawezi kutuondoa. Trust me. Game ya kwanza tulitoa sare ya 1-1 Kule kwao Roma. Leo tupo home awike, asiwike kutakucha. Fainal ni cc na nyie. Over!
Ntuzu huwa unaangalia game za Juventus au wewe ni EPL tu Mkuu? Nasikia mnamtaka sana Pogba, tupeni Oscar na pesa tuwape the Pogboom
Tuna kijana anaitwa Pereyra, umemuona huyo?
Hua naangalia mkuu Mara moja moja sn.
Oscar hawezi kutoka pale Chelsea ila tunaweza kumng'oa Pogba kwa hela tu
Hata Violla walibahatisha kaushindi pale home, dhahma ikawakuta mbele ya wake zao na wakwe zao, sasa wewe endelea kukariri kuwa utashinda kwa sababu kigodoro kinapigwa gheto
Hivi mna mechi ngapi hamjashinda?
Vyovyote vile, mtuletee £75m tukamchukue Ilkay Gundogan, RVP na vijana wa kiamerika wengine kama watatu hivi
Sasa akija huko atacheza namba ya nani?
Atacheza nafasi hiyo hiyo anayocheza huko
Umenijibu kama mtu asiyejua soka Ntuzu
Sisi Bianconero tunacheza mfumo tofauti na Chelsea, na hata mfumo ukibadilishwa kutokana na mpinzani, kiuongo yetu huwa na kiungo wa chini (St.Andrea Pirlo/Mpiganaji Marchisio) na mbele yake anakua na vioungo wengine wawili, mara nyingi hawa ni Vidal na Pogba, pembeni kule kuna wing backs na washambuliaji pacha
Nyie mnacheza 4-2-3-1, kwa uchezaji wa Pogba na ukitaka umfurahie huyo dogo, kuna namba mbili tu za kucheza hapo kwenu, ya Fabregas au Oscar, and you can't leave a £75m signing on the bench, can you?