Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

Yaani hii ni juve mbovu kuliko misimu iliyopita chini ya Allegri. Huko Italy kwenyewe alipigwa tatu bila na Atalanta na kutolewa kwenye copa italy.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo kubwa la Juventus ni ujio wa Ronaldo, Wachezaji wengi wa mbele wamekua wakicheza chini ya kiwango toka atue Ronaldo, Mana mfumo mpya unawalazimu kumtumikia Ronaldo na wanakua hawapo huru kabisa. Masikini Dybala na Costa wamekua wakicheza kwenye wakati mgumu sana.
Niliwahi kuzungumza nikaishia kutolewa povu humu. Kama Ronaldo hatoisaidia Juventus bali ataibovua. Usajili wake haukuhitajika kabisa kwenye timu. Pesa ilikua itumike kuimarisha midfield mana wazee kina Khadira na Pijanic wameshachoka. Ila wakaishia kuingizwa mkenge kwa mihemko yao.
 
Na leo imezikwa rasmi.... Shida hakuna ushindani Serie A timu imebweteka ndio maana tokea christmas mpira mbovu sana wanacheza kibaya zaidi wanataka kumsajili na Icardi msimu ujao!! Yaani kwa mtindo huu wa kuunda monopoly serie A mashindano kma UEFA mtaendelea kuyasikia redioni tu.

Acha visababu visivo na msingi. Juventus msimu huu ni ovyo kabisa, hata huko Serie A wanashinda ushindi wa kusuasua. Wamekula kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Atalanta majuzi tu.
Timu ina matatizo ya midfield na wanashindwa kulitatua wakaishia kutoa mamilioni kwa mchezaji ambae anasubiria Penalt tu uwanjani.
 
Hahahaha naona una hasira na Ronaldo kuwakimbia hadi Madrid mmebaki yatima kabisa..... All in all shida ni ligi kukosa ushindani sidhani kma Ac milan na inter + Roma zikiwa top form kama juve angesuasua hivi. Hata spain Bila uwepo wa Atletico + Barcelona nyie Madrid msingekuwa serious kabisa ila changamoto za domestic league zinawapa incentive ya kuzoea mapambano ndio maana mkadominate UEFA.

Hii shida ipo France na Germany pia wachezaji wote wazuri wanarundikana Psg na Bayern ndio matokeo wameua ligi zao wenyewe.
 
Penaldo mkuu
Ila alivyokuwa kwenu hakuwa Penaldo?? Tuwe wakweli tu pengo la Ronaldo bado linawatesa na itawachukua miaka kurudi kwenye ubora wenu kama ndio mnategemea hivo vitoto kina Asensio na Lucas!!
 
Ila alivyokuwa kwenu hakuwa Penaldo?? Tuwe wakweli tu pengo la Ronaldo bado linawatesa na itawachukua miaka kurudi kwenye ubora wenu kama ndio mnategemea hivo vitoto kina Asensio na Lucas!!

Acha kuropokwa, Real ipo kwenye right track. Ila hao Juventus ndio wanaoteseka
 
Hahahaha naona una hasira na Ronaldo kuwakimbia hadi Madrid mmebaki yatima kabisa..... All in all shida ni ligi kukosa ushindani sidhani kma Ac milan na inter + Roma zikiwa top form kama juve angesuasua hivi. Hata spain Bila uwepo wa Atletico + Barcelona nyie Madrid msingekuwa serious kabisa ila changamoto za domestic league zinawapa incentive ya kuzoea mapambano ndio maana mkadominate UEFA.

Hii shida ipo France na Germany pia wachezaji wote wazuri wanarundikana Psg na Bayern ndio matokeo wameua ligi zao wenyewe.

Narejea tena mkuu iyo sio hoja, Ni hoja dhaifu inayopaliliwa na waingereza kwa kujaribu kuaminisha dunia kuwa wao ndio wana ligi Bora. Mana hoja hio huwezi kuikuta popote zaidi ya vyombo vya habari vya kiengereza tu. Hata huko La liga utasikia ni ligi ya timu mbili.
Sasa kama kuwa na ligi ya ushindani ndio nguzo kuu ya mafanikio ulaya, basi kwa tunavoaminishwa kuwa England ndio kwenye ligi bora mbona timu zao ni vilaza? Buyern, Juve na PSG wakiekewa timu yoyote yakiengereeza kwenye makweli wanaziangamiza.

Hata ukisikia Juventus, Buyern, PSG wametolewa mashindano ya Ulaya basi ujue wametolewa na Barca, Real au Atletico hakuna wengine.
 
Acha kuropokwa, Real ipo kwenye right track. Ila hao Juventus ndio wanaoteseka
Right track gani mkuu hivi kweli nyie ni wakupigwa na Girona bernabeau!! Yaani Ajax ndio wakuwakimbiza vile?? Ngoja hiyo El clasico ifike ndio utaelewa nachosema sahvi mkipigwa 10 ndio utakiri kuna shida tena kubwa sana.
 
Real Madrid tayari ameshatia mguu mmoja ndani ya Champion league Quarter final. Juventus washaelekea kuchinjwa halafu bado unataka kipi chengine?
 
Real Madrid tayari ameshatia mguu mmoja ndani ya Champion league Quarter final. Juventus washaelekea kuchinjwa halafu bado unataka kipi chengine?
Kama ajax inakutoa jasho vile basi ukikutana na timu ''serious'' walau Spurs ama Roma ndio itakuwa kipimo sahihi na kujua shida kubwa iliyopo Real.
 
Narejea tena mkuu iyo sio hoja, Ni hoja dhaifu inayopaliliwa na waingereza kwa kujaribu kuaminisha dunia kuwa wao ndio wana ligi Bora. Mana hoja hio huwezi kuikuta popote zaidi ya vyombo vya habari vya kiengereza tu. Hata huko La liga utasikia ni ligi ya timu mbili.
Sasa kama kuwa na ligi ya ushindani ndio nguzo kuu ya mafanikio ulaya, basi kwa tunavoaminishwa kuwa England ndio kwenye ligi bora mbona timu zao ni vilaza? Buyern, Juve na PSG wakiekewa timu yoyote yakiengereeza kwenye makweli wanaziangamiza.

Hata ukisikia Juventus, Buyern, PSG wametolewa mashindano ya Ulaya basi ujue wametolewa na Barca, Real au Atletico hakuna wengine.

Ligi bora SPAIN
Ligi maarufu UINGEREZA
Ligi ya wakulima FRANCE
 
Mkuu upo?? Naona leo Juve imefundishwa mpira wa ushindani sio yale mabonanza mliyozoea kucheza huko Italia sijui cagliari na chievo!! Poleni sana jaribuni tena bahati mwakani maana Huko Turin tegemea Simeone kupaki basi mwanzo mwisho.
Naona umeiwekea Mdhamana Athletico ila nakupa pole maana atatoroka na jela utaingia wewe... Athletico ni wahuni fulani usiwaamini shauri yako ni kama Westhama tu wale.... Juve imefunzwaje Mpira wakati game waliitawala yote Hadi Griezzman aligeuka beki mkuu

Juve na ManU Lazima zitacomeback tu wala usikhofu..
 
Mimi ni shabiki mkubwa wa Juve.Sioni tatizo kwa Ronaldo bali naona matatizo kwa timu.Tempo ya UCL haipo kwa Juve mwaka huu,wapo wapo tu.
Defence imebomoka,set plays zinaisumbua ngome ya juve tangu Allegri awe kocha.Mipira ya juu ni shida kwao pia.
Hawachezi kwenda mbele,wanapenda possesion tu na goli lije lenyewe au kwa chance,mpira wa kuvizia,sio pressing.Hili ni tatizo.Hii sijui ni mara ya ngapi naona Juve inacollapse kadri dk zinavyokwenda.
Midfield hakuna na ni tatizo la siku nyingi tangu akina Vidal waindoke,sijui kwanini wanaendelea kulipotezea ilhali linawagharimu sana.
Style ya uchezaji ya Italia inawafanya Juve na timu nyingine za huko kushindwa kuperfom ulaya.They need to switch from tactical gameplay to tactical and technical aspect intergrated.
Pia kuna kitu cha ajabu ambacho sijakizoea kwa italian teams nakiona kwa Juve.Hawako agressive.Wakikutana na timu zinazotumia nguvu na kuchapa kiatu Juve hupata wakati mgumu.ni kujiangusha tuu muda wote na kutafuta huruma za refa.Very stupid!Hili sijalizoea kabisa kwa wataliano,weka hapo Canavaro,Thuram,Zambrota,Zidane,Davids,Cafu,Maldini,Deschamps,Simeone,Conte,Materazzi,Gatuso,Ferrara,Maradona,De Lima n.kHatukuzoea ujinga huu Serie A!ilikuwa kazi kazi!Hii Juve inatoa wapi huu uchezaji laini?!Ni Cancelo,Bernadeschi,Cuadrado kidogo na Ronaldo ndio at times wako aggresive ila the rest of team hata sijui wana pepo gani!Mandzukic hatabiriki,mara yupo mara hayupo.
Mwisho nadhani imefika mahali Juve iagane kwa amani na Allegri.Kafikia ukomo,he have nothing new to add.
Natamani kuona kipara cha Zizzou pale Allianz halafu Materazzi akamtembelee😀
Ikishindikana basi achomolewe Deschamps kule ufaransa,au tukaibomoe Liverpool tumchukue mawani,au tukamshawishi yule babu wa Bayern Jup Heynckes kwa muda.Ila hali ni tete.
Kumpiga Atletico second leg,inahitajika Juve nyingine kabisa kama ya zamani,sio hii ya recently.
 
Mm naamini juve ikitulia itapindua matokeo ndani ya Turin. Shida ya juve ipo kwa viungo na mabeki. Ukimtoa pjanic juve hawana kiungo anayeweza kuichezesha timu vizuri. Unamwachaje benatia na Caldara waondoke wakati unatambua bonucci na chielini wamebakiza mwaka kumaliza soka lao. Kwa mpira wa leo unapowapanga mabeki wa pembeni halafu wanashindwa kupiga cross hata moja ni tatizo hilo. FINOALLAFINE
 
Bologna 0 Juve 1,La Joya kaokoa jahazi.Kwa kweli Juve kwa mpira huu wajiandae kupigwa tena na Atletico.Zile Counter attack za Atleti zinaweza kumvua chupi mtu mzima chumbani kwake aisee!Poor attacking tactics,sijui nini kimewakuta aisee.Bologna wamewabana vilivyo.Allegri must go.Tusidanganyane.
 
Hata hujakosea mie ni Team atletico since back then na kukuonyesha kuwa ligi bora hutengeneza timu bora za UEFA angalia timu za hispania kudominate UEFA kule Europa walibeba sevilla mara 3 mfululizo na Champions league walibeba madrid mara 3 mfululizo na yote ni sababu ligi yao iko competitive sana... sasa vitu kama hivi huwezi kuvikuta Italy maana ligi ya ndani hakuna ushindani umemalizwa na juve.

Unaposema atletico ana kimavi ur kidding right?? Mind you amechukua Europa na super cup kwa kuidungua Real timu ambayo juve mmeishindwa kwa recent UEFA matches sasa nani hapo ana kimavi juve au atletico?? Juve mara ya mwisho kubeba hata UEFA cup ilikuwa mwaka gani?? Bajeti ya atletico haifikii robo ya bajeti na gharama za usajili za juve ila wana uefa super cup 3 na Europa ligi 3 ndani ya decade hii then unasema wana kimavi??

Mie nlikuwa mshabiki sana wa Serie A enzi hizo Italia moto kuanzia Parma ya kina cannavaro mpaka Hellas verona ya Adrian mutu.... Hapo kuna Inter ya zamorano na AC milan ya kina Baggio moto usipime sio cku hizi timu moja tu mmeua mpira

Hapo unakuta msimu ujao Icardi,Under na Piatek wanahamia juve..... Narudia tena RIP Serie A na kwa tabia hii subirini kipigo kutoka atletico maana wao kila mechi spain ni competitive hivyo UEFA haiwashindi ila kazi kwenu msiozoea ushindani mtanyooshwa tu maana hakuna namna

Poleni sana
Naona maneno yako leo utayanywa
 
Back
Top Bottom