Well,mie nadhani Conte yupo sahihi ila ameongea kwa ukali sana,nasikia hadi Agnelli amemuita na kumtuliza asibishane na "watu wazima",Capello nakubaliana naye upande mmoja kwamba serie a imeshuka kiwango,lakini upande mwingine anaposema kiwango hicho kimeshuka kiasi cha kuathiri perfomance ya Juventus ulaya,hapo sikubaliani naye kabisa.Juve hawana weakness yenye ukubwa wa kushindwa kuwazuia kufika quarterfinals za ulaya.Kutolewa mapema mwaka huu si tatizo la competency ya timu,uwendawazimu na loss of concentration ambayo timu kubwa kama Juve huwa hawairudii mara kwa mara na mtu yeyote akilichukulia hili kudetermine kiwango cha Juve msimu ujao atakosea.Tuangalie how Juve went out,draw ya kule Denmark,kweli tulitoka draw kwa kushindwa kiviwango kwenye mechi ile?hapana.Draw ya Turin dhidi ya Galatasaray,kweli tulipata sare ile kwa ajili ya kuzidiwa kiwango na Galatasaray?hapana,ni upuuzi wetu wenyewe ulitucost,mechi mbili dhidi ya Madrid,tuwe wakweli(na Madrid ni wakubwa),kuna mechi yoyote unayoweza kusema Juve alizidiwa?hapana,bahati tu ilikuwa kwa Madrid na hasa ile mechi ya Bernebeu kama tusingepigwa ile red..sijui!mechi ya mwisho dhidi ya Galatasary ushindi ule ni wa mezani kwa sababu ile haikuwa football,huwezi kucheza mpira kwenye tope,hata Bayern angeweza kufungwa,ilikuwa fluku fluku tu na wale waturuki wana style ya mipira mirefu,ikawa advantage kwao dhidi ya Juve inayocheza mpira wa kutandaza chini kwa mpangilio,mpira wao ukafia kwenye madimbwi,that was completely unfair achilia mbali mpira kuchezwa two days nusu nusu,that game was UEFA's biggest shame hata goal.com waingereza wanaosifika kuikandia serie a na timu zetu walitoa editorial wakikandia vibaya uamuzi wa UEFA kuchezesha ile mechi,that wasn't football,because you can't apply football rules and techniques in water and mud!that was crazy aisee!kila mtu aliwashangaa hadi viongozi wa Galatasaray wenyewe walisema mechi haikustahili kuchezwa!sasa nikiyatazama haya,na kumbukumbu za kumtwanga Chelsea,Celtic,Shaktar na kuja kutolewa na Bayern iliyotwaa ubingwa,sidhani kama Juve ni dhaifu hivyo anavyosema Capello.Napoli?kwa matokeo yao misimu miwili iliyopita sidhani kama ni dhaifu,hao Totenham wenyewe walitoka jasho kwa Lazio,sembuse Juve?Huyo Atletico asitegemee mteremko kwa Milan hata kidogo!what about Roma?ni timu dhaifu ile?Capello amekosea hapa.Serie a imekosa wachezaji bora "wenye majina" na si wachezaji bora.Halafu kushuka kiwango cha serie a kwa margin hii ya sasa bado si excuse kwa Juve kufanya vibaya ulaya.PSG wanatoka ligi gani?mbona wapo wapo sana tu ulaya?Basel?what about Bayern huko nyuma waliendelea kuwa established force ulaya pamoja na Bundesliga kushuka kiwango miaka ile.How did they manage that?ni kuichukulia ulaya kama nchi yenye ligi yake,ukatumia advantage ya kuwa regular champion kwenye nchi yako kushiriki ulaya kila siku,ukatumia pesa unazopata kuendelea kukandamiza wanyonge wako huko kwenu huku ukijenga kikosi kitakachokuwa cheap financially and strong tactically and technically,avoid many big names(just take few) and take quality players with no names,grow up with them(sio kubadili sera very early unapoona fedha zinaanza kujaa,)that's what Barcelona did 8 to 10
years ago kuwaondoa akina Kluivert na Enrique na kuwachukua akina Ronaldinho wanaochipukia,that's what TP Mazembe is doing,that's what Bayern did and that's what Juve is doing now na naamini watafanikiwa kama hao wengine.Kwa hiyo kushuka kiwango serie a haiwezi kuwa excuse kwa Juve kubweteka na kusema "jamani,ligi yetu mbovu,hatuwezi kufanikiwa ulaya".Ingekuwa hivyo basi ningewashauri waje vodacom premier league tu manake huku ndiko kwenye watu wenye visingizio na si solutions for success no matter what!