Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Staa wa muziki, Jux, amerudi bongo usiku wa kuamkia leo, Septemba 5, akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mpenzi wake Priscilla Ajoke, mtoto wa mwigizaji mkongwe Iyabo Ojo kutoka Nigeria.
Hivi karibuni, wawili hao walikuwa Nigeria wakijirusha kwenye party ya birthday ya Jux, na sasa wamefika bongo fresh na vibes zao za kimahaba zikizidi kunoga.
Baada ya kutua Tanzania na kupokewa na wanawe, Jux ameweka wazi kuwa anaelewa onyo alilopewa na baadhi ya Wanigeria kumhusu mpenzi wake, Priscilla, akisema wanamlinda kwa sababu ya historia yake ya mahusiano na wanawake waliopita, pamoja na umaarufu wa Priscilla nchini Nigeria tangu utotoni, hivyo ni kipenzi chao na wanamlinda kwa upendo huo.
Priscilla amekuwa maarufu Nigeria tangu akiwa mdogo, hivyo ana nafasi ya pekee mioyoni mwao, na ni wazi kwanini wanahisi haja ya kumlinda kwa nguvu hizo.
Jux amesema ilikuwa moment nzuri na alifurahia kila kitu kilichotokea Nigeria na kuhusu kumvalisha pete ya uchumba amesema hilo bado watu wasubiri kwa sasa.