Jux ajibu onyo la Wanigeria, akana kumchumbia Priscilla

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Staa wa muziki, Jux, amerudi bongo usiku wa kuamkia leo, Septemba 5, akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mpenzi wake Priscilla Ajoke, mtoto wa mwigizaji mkongwe Iyabo Ojo kutoka Nigeria.

Hivi karibuni, wawili hao walikuwa Nigeria wakijirusha kwenye party ya birthday ya Jux, na sasa wamefika bongo fresh na vibes zao za kimahaba zikizidi kunoga.

Your browser is not able to display this video.
Baada ya kutua Tanzania na kupokewa na wanawe, Jux ameweka wazi kuwa anaelewa onyo alilopewa na baadhi ya Wanigeria kumhusu mpenzi wake, Priscilla, akisema wanamlinda kwa sababu ya historia yake ya mahusiano na wanawake waliopita, pamoja na umaarufu wa Priscilla nchini Nigeria tangu utotoni, hivyo ni kipenzi chao na wanamlinda kwa upendo huo.

Your browser is not able to display this video.
Priscilla amekuwa maarufu Nigeria tangu akiwa mdogo, hivyo ana nafasi ya pekee mioyoni mwao, na ni wazi kwanini wanahisi haja ya kumlinda kwa nguvu hizo.

Your browser is not able to display this video.
Jux amesema ilikuwa moment nzuri na alifurahia kila kitu kilichotokea Nigeria na kuhusu kumvalisha pete ya uchumba amesema hilo bado watu wasubiri kwa sasa.

 

Attachments

  • ssstwitter.com_1725517827949.mp4
    11.6 MB
  • ssstwitter.com_1725517825552.mp4
    15.3 MB
  • ssstwitter.com_1725517822004.mp4
    8.7 MB
  • ssstwitter.com_1725517780336(1).mp4
    6.2 MB
  • 1725518407871.jpeg
    228.3 KB · Views: 10
Siku hizi nikiingiaga jf nakuja kufanya reference dah kuna uzi nautafuta wambea hii kapo si mwaka mmoja tu au mnasemaje?

Huo umbea kama haukuandikwaga na marehemu warumi basi ni mmbea mwingine. Wacha niendelee kufukua makaburi humu.
 
Ila huyu demu Kwa muonekano wa nje mkali sana, kwa ndani labda nikabidhi maiki Kwa mashujaaa wa jf wenye uzoefu wa miaka 20++ katika tasnia ya kuslide wamuelezee..... karibuni sana
Mkali mnoo na kanaonekana bright huwa ni mara chache nafanya maombi kwa Hawa celebrities maana maisha Yao maigizo ila kwa Hawa naomba sana wawe kama Don Bill na Nandy
 
Jum lokole kama Jux Chama moja
 
Nenda Iraq ukawauzie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…