JWTZ: Baada ya siku 7 atakayepatikana amevaa, anatumia au anauza mavazi ya Jeshi atapatiwa adhabu kali

Wewe badala ya kutetea dhuruma unaisifia! Nguo hizo zimeingizwa kihalali na zimelipiwa ushuru TRA baada ya kujiridhisha ni mali halali.
 
Vaeni mpendeze na nyinyi si wazalendo, Kuna ubaya gani ?
 
Nadhani Jeshi letu linahitaji uvuvio.
 
Na haya mashitaka ya uhaini, na mijadala ya DPW, isijekuwa tayari kawekewa mtu shehena ya hayo magwanda ili aingizwe king!
 
Wale nao wanapenda ujiko wa kizamani sana.

Depo siku mbili tayari anajiona kashakuwa Rambo.

Hao wanaokurukisha vichura haina maana wao hivyo vichura wanaviweza.

Ngoja nikupe stori moja.

Kuna mwanangu alikuwa ameenda jeshini.

Wiki mbili za mwanzo walikusanyika wageni wote waliowasili hapo jeshini kwa ajili ya mafunzo.

Kisha mkuu wa Kambi akamteua kijana mmoja kutoka kwenye kikosi chake ambacho kina uzoefu wa kutosha wa mazoezi hapo kambini.

Yule kijana kutoka kwenye kikosi chenye uzoefu akapewa kazi ya kuwa train hawa new comers.

Basi jamaa akawa anawapa mazoezi magumu hawa new comers, kutokana na ugumu wa mazoezi na ugeni jamaa wakawa wanalia, ye mchizi anawacheka huku akiwaambia hili ndio jeshi mkiwa manyumbani mnafikiriaga ni rahisi eeh

Sasa siku moja nasikia yule kiongozi Mkuu wa kambi akawaunganisha wale new comers na wale expert kwenye gwaride la pamoja.

Halafu akawapigisha zoezi moja kali. Basi si unajua muda unavyozidi kuchanganya ndio zoezi linazidi kukolea.

Wakiwa katikati ya zoezi wakaanza kusikia sauti ya chini kama kuna mtu analia.

Kadri zoezi linavyozidi kuchanganya ndio ile sauti inavyozidi kuongezeka.

Kugeuka nyuma kuangalia nani anayelia wanashangaa kumuona yule masta wao aliyekuwa anawafundisha analia hadi mikamasi inamtoka.
 
waache kuishi maisha ya kijima sasa ni mwaka 2023 sio mwaka 1980
 
Jeshi la Wananchi ( JWTZ) limetoa Siku 7 kuanzia leo 24/08/2023 kwa Wananchi Wenye Mavazi ya Jeshi au yanayofanana na Sare za Jeshi kuyasalimisha Jeshini baada ya Siku 7 Msako mkali Utaanza nchi nzima

Source: Ayo tv
 
Bora watarudisha heshima ya Jeshi. Unakuta limtu Lina miguu yote ya kushoto, halijawahi kucheza hata sungu sungu achilia mbali mgambo, lisanii mara la hip hop au taarabu linakwenda kufananisha Mavazi ya majeshi yetu. Hata kama ni rangi za majeshi ambayo sio ya nchi yetu umeyakuta kwenye mtumba unayanunua ya nini? Si ununue zinazoendana na wewe? Nadhani majeshi yote yaungane kuwasaka wanaofananisha nguo zao ama kwa rangi ama kwa mishono. Mbona hawaigi nguo za wafungwa au manesi?
 
Those are trivial things. Defence force can do better than this.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…