Kama wanaongelea kufuata sheria, na wanasisitiza hivyo, basi Jeshi linapaswa kuwa mfano wa kufuata hizo sheria. Kwa kuanzia waanze kwa kupeleka malalamiko yao Polisi.
Polisi ndiyo wenye mamlaka ya kufuatilia hilo, waachane na jungle minds, zama zimebadilika hizi wanapaswa kujua majukumu yao yanapoishia. Tunalipenda na kuliheshimu Jeshi letu, so linapaswa kutambua misingi, sheria kanuni na mipaka ya majukumu yao.
Kwa Jeshi kupeleka malalamiko yao Polisi, siyo unyonge, bali itadhihirisha kuwa ni Jeshi linalojitambua, na linalotambua majukumu yake na ya wengine, na mipaka yake, zaidi itaibua hali ya Wananchi kufuata sheria na kwamba kumbe kufuata sheria siyo unyonge au utumwa bali ni ustaarabu na kujitambua.
Nguvu za hizi taasisi zinaundwa kutokana na sheria. Uhamiaji ilikua ni idara tu, sasa hivi baada ya muswada kupitishwa na kuwa sheria, Uhamiaji hivi sasa ni Jeshi kwa mujibu wa sheria iliyoliunda, na kuna sheria zinazoelekeza aina ya silaha wanazopaswa kutumia wawapo kazini, pia wanazoruhusiwa kuwa nazo popote hata majumbani.
Sheria ndiyo inaelekeza aina ya mafunzo gani yatolewe kwa Jeshi lipi, siyo kwa sababu labda Jeshi fulani ni noma kuliko lingine.
Sheria ikibadilishwa inaweza kupelekea JW inakua Polisi na Polisi wakawa JW. Tuachane na jungle minds, those days are long gone.
Mkuu hongera kuwa open minded.
Huu mjadala siyo mpya, wala matamko ya Jwtz kuhusu mavazi yenye kufanana na sare za jeshi siyo mapya, huibuliwa na kusinyaa kwa sababu si ya kisheria, huu ni mwendelezo tu wa ubabe wa kunyanyasa raia.
Huyo mwanajeshi aliyesimama kwenye mimbari kutoa msimamo huo wa jeshi kuhusu jambo hilo, hakuandaliwa.
Nimesema hivyo kwa sababu, maswali yote muhimu aliyoulizwa na waandishi wa habari ambao ni ma lay man katika masuala ya kijeshi hakuyajibu ipaswavyo kiweledi ama aliyakwepa.
Mimi hapa nitajikita katika mambo kadhaa kwa kuwa siyakumbuki yote yaliyoongelewa:
La kwanza na la muhimu likiwa ni mapungufu ya wazi ya kisheria katika jambo hilo.
Katika kumiliki haki ya bidhaa(brand)yoyote, kuna process za kufuatwa ili mtu ama taasisi kupata haki miliki.
Jambo hilo linafahamika na sitalielezea.
Je Jwtz ina haki miliki ya mavazi wanayoyatumia kwa sasa ambayo wanaagiza tu kupitia mzabuni yeyote ambaye huyanunua popote kutoka kiwanda chochote cha ndani ama nje ya nchi?
Je ni rangi gani ama maua gani ya mavazi ambayo rasmi kisheria yanayotajwa kuwa ni ya jeshi katika context yake hiyo?
Na ni jeshi gani aliloliongelea yeye?
Labda tumkumbushe taratibu ambazo kwamfano sare gani za Jwtz zivaliwe ambazo hufuatwa, yeye msemaji hakuzielezea!
Katika sheria za kijeshi, The Defence forces regulations Vol.1, zimeeleza wazi kuwa sare zinazovaliwa na staff wa Jwtz kwa wakati husika kibali chake hutolewa na mkuu wa majeshi.
Kwa hiyo wanavyoonekana leo, kesho waweza kuta wamebadilishiwa kutokana na matakwa ya mkuu wao wa majeshi(Cdf) na bila majadiliano yoyote.
Pia katika The Defence forces regulations vol.1 hiyo, Sheria zinajibu swali la mwandishi wa habari kuhusu wasanii na waigizaji, ambalo yeye alishindwa kulijibu.
Ni kwamba wasanii ama waigizaji wanapotaka kutumia mavazi ama vifaa vya kijeshi kuigizia,sheria zinawaelekeza wapeleke maombi yao Makao makuu ya jeshi kwa kibali period!
Sasa mitaani kwenye maduka ya nguo kumejaa vitambaa vyenye rangi mbali mbali ambazo zinatumiwa na majeshi yetu, vikiwemo vya kijani, vyeupe, blue, vyekundu na vyeusi vinavyotumiwa na wanajeshi.
PT na uhamiaji ni vyeupe, blue, khaki na jungle green.
Ugoro na kijani wanavyotumia MT nk nk.
Kwa hiyo rangi zote za maana wameziwin wanajeshi, sasa sisi raia tuvae rangi gani sasa!
Je kutoa tamko la jumla jumla haoni kwamba analeta mtafaruku kwa wafanya biashara wa nguo nchini?
Je marobota ya nguo hizo yakizuiliwa kuuzwa ni nani atakayefidia hasara hiyo?
Hiyo sheria anayoitetea ama "makosa" aliyokemea yameanza leo?
Kwanini kipindi hiki?
Au kwa sababu hivi karibuni Mbowe alionekana kuhutubia kwenye mkutano flani, nyuma yake kasimama mtu kama mpambe katinga gwanda?
Je tukisema Jeshi letu limeanza kujiingiza kwenye siasa ama kutumiwa na wanasiasa watasemaje?
Suala la mavazi ni mtambuka, asilione lirahisi namna hiyo, maana linagusa mpaka uchumi wa nchi ajue!
Hivi kufanya uhalifu ama mhalifu anaweza kuvaa sare za kijeshi mchana bila ya kugundulika kirahisi?
Au raia lay man anaweza kuvaa vazi la kijeshi na kujfanya mwanajeshi, yaweza pita kutwa nzima hajadakwa?
Uanajeshi siyo mavazi tu, ajiulize concentration ya vita namna wanajeshi wasiofahamiana ambavyo hukusanywa na kuchanganywa pamoja kumkabili adui, hufahamiana kwa mavazi pekee?
Kitu gani huwafanya watambuane?
Jamani acheni raia wema wajivalie mitumba yao waliyoinunua kwa jasho jingi.
Kwa wapenda makesi wakiingia kizimbani kwa issue kama hizi hakuna sheria hapo itakayo waadabisha.