Nauliza tu…
Mara nyingi sasa tumeziona mbwembwe za makomandoo wa JWTZ.
Tumeona jinsi wanavyovunja matofali kwa mikono.
Tumeona jinsi wanavyovunja vibao kwa mateke.
Tumeona jinsi wanavyobeba mabegi ya mgongoni makubwa na mazito.
Pia, tumeona na kumsikia msemaji wa jeshi letu akisema kuwa jeshi letu ni moja ya majeshi bora 6 duniani 🤣.
Sasa, kwa ufahamu wangu mimi, majeshi yote yaliyo bora duniani yana vitengo vya cyber warfare.
Wiki hii tumeshuhudia moja ya kazi za kitengo cha cyber warfare huko Lebanon.
Ingawa hawajakiri kuwa ni wao, lakini watu wengi wenye akili wana fununu kuwa ni akina nani hao waliohusika na kuzilipua pagers za Hezbollah……IDF kupitia kitengo chao cha cyber warfare.
Sijui Kama JWTZ wana hicho kitengo. Sina hakika kama wana uwezo hata wa kudukua mifumo yoyote iliyopo Burundi au hata Sudan ya Kusini.
Kwa mnaojua, JWTZ wakoje kwenye hayo mambo?
Jeshi letu lipo vizuri sana sana .
Tatizo ni moja kama zilivyo taasisi zote za serikali .
CCM imeingiza watu wa hovyo kila idara na kuwapa mamlaka ya juu kwa ajili ya kulindana na kuliibia Taifa tuu.
Sasa kinachofanyika ni kuhakikisha wale wanaootoa mawazo tofauti wanaitwa wapinzani na mara nyingi wanauawa au kufukuzwa au hawapandishwi vyeo wala kupewa idara za kuongoza . Matokeo yake idara zote za serikali zinaongozwa na ama watu wenye Elimu ya kununua au kupewa tu kama tunavyoona wale wanasiasa wengi ni madokteri wa kununua kwenye vyuo ambavyo ni wadau wao na walioweka tena wakuu wa hivyo vyuo ni watu wao wa kutengeneza fikra za kudumisha chama na kuzalisha machawa.
Jeshi letu lina kiwanda cha magari pale nyumbu.
rais .
Jeshi lipo chini ya ni kwa nini tunashindwa kuzalisha malori na magari hata ya kuzoa Taka .
Tulitegemea vyuo vyote vya kijeshi vinunue malori kutoka nyumbu kwa ajili ya hata kubeba vyakula na mikate JKT.
Watakua na sayansi gani kama wanakua na hamira Jeshini Mkubwa anayewaweka stendi bai muda wote kupambana na Mbowe na Lisu.
Yaani Jeshi wanatolewa lakambini kwenda kufagia barabarani kwa ajili ya kuzuia Wananchi wasiandamane kupinga kutawaliwa na Raia madikteta wanaoongoza nchi Kijeshi.
Nyerere baba wa Taifa, Mwinyi Mkapa ,Kikwete luteni Kanali lakini hawajawahi kuvunja sheria kwa kuvaa nguo za Jeshi.
Hawa Majambazi hatujui wamepata wapi Uniform za Jeshi wanavaa bila aibu.
Nani anawashauri , bila shaka ni wale Makada waliowachomeka kule.
Hawa wakubwa mle ndani hawawazi teknolojia wanawaza kutumia jeshi kulinda CCM. Hawaoni kuwa siku akitokea adui wa nje tutapigwa mana hata umoja wananchi wa ndani haupo tena kutokana na watu kuumizwa na Hamira Jeshini mkubwa.
Hawajui iko siku watoto wa maskini watakataa kuwapiga ndugu zao kama matofali.