Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nauliza tu…
Mara nyingi sasa tumeziona mbwembwe za makomandoo wa JWTZ.
Tumeona jinsi wanavyovunja matofali kwa mikono.
Tumeona jinsi wanavyovunja vibao kwa mateke.
Tumeona jinsi wanavyobeba mabegi ya mgongoni makubwa na mazito.
Pia, tumeona na kumsikia msemaji wa jeshi letu akisema kuwa jeshi letu ni moja ya majeshi bora 6 duniani 🤣.
Sasa, kwa ufahamu wangu mimi, majeshi yote yaliyo bora duniani yana vitengo vya cyber warfare.
Wiki hii tumeshuhudia moja ya kazi za kitengo cha cyber warfare huko Lebanon.
Ingawa hawajakiri kuwa ni wao, lakini watu wengi wenye akili wana fununu kuwa ni akina nani hao waliohusika na kuzilipua pagers za Hezbollah……IDF kupitia kitengo chao cha cyber warfare.
Sijui Kama JWTZ wana hicho kitengo. Sina hakika kama wana uwezo hata wa kudukua mifumo yoyote iliyopo Burundi au hata Sudan ya Kusini.
Kwa mnaojua, JWTZ wakoje kwenye hayo mambo?