Echolima
JF-Expert Member
- Oct 28, 2007
- 3,824
- 2,079
Mtoa mada wewe ni mwongo sana na una nia ya kutisha watu bila sababu ya maana,huo ni UZUSHI mkubwa umeleta.
Nimeipata katika nchi jirani iliyokua na vita ya maneno na Tanzania, miaka ya karibuni kumekuwa na hujuma kubwa inafanywa ndani ya JWTZ hasa katika mfumo wa mafunzo kwa kada chini yaani JRN NCOs n SRNCOs katika vyuo vyao.
Swala liko hivi, kitengo cha kijasusi cha nchi hiyo kilituma mawakala nchini kiliwalenga wakuu wa vyuo hivyo vilivyopo TABORA KALUNDE, ZANZIBAR CHUKWANI, DAR ES SALAAM KIMBIJI mawakala walikua na kazi moja tu yakushawishi kulegeza mafunzo ya kijeshi na nidhamuili kuzoletesha ufanisi na utendaji kivita kwa JWTZ na wakuu hao wa vyuo wanafaidika na mgao mkubwa wa fedha toka katika nchi hiyo.
Kinachofanyika ili kutakatisha fedha hiyo wakuu hao hupitisha michango kwa wanafunzi wanaohudhuria kozi ktk vyuo vyao kwa kichwa kimoja huweza kufikia tsh 300000 hadi tsh 500000 kwa mda wa miezi minne ambayo hukaa hapo.
Kumbuka chuo kimoja huchukua wanafunzi kati ya 400 hadi 1000 elfu moja hukusanya zaidi ya tsh 100 millioni mia moja ambazo hazina ukaguzi wowote kwa kisingizio cha ujenzi wa miundo mbinu au huendesha klub za michezo hapo ndio kitendawili kilipo haijulikani kiasi wanakusanya na zinatumikaje sababu huzungukwa na mazingira ya usiri sana.
Pia hili hufanyika kama syndicate mtandao huu upo hadi makao makuu ya jeshi kila mtu hupata kutokana na ushiriki wake, mfano kurugenzi ya mafunzo hushurutishwa kupeleka idadi kubwa ya wanafunzi kuliko miundo mbinu ya vyuo husika lengo ni kupeleka nguvu kubwa kwaajiri ya kupata michango na mgao kwa kila moja ili kufanikisha hayo mambo yafuatayo hufanyika.
1. Chuo hupokea idadi kubwa ya wanafunzi bila uwiano sawa na wakufunzi kwa hili chuo kilichoathirika sana ni Kalunde TC
2 Wakufunzi hasa maofisa waandamizi wanaonekana kua na misimamo ya kukinzana na wakuu hao wa vyuo huamishwa vituoni mara moja na kupelekwa sehemu zingine ili kupunguza makali ya kozi.
3 Hufanya jitahada za makusudi kulegeza mafunzo ili kutoa ushawishi kwa wanafunzi kutoa michango bila malalamiko hili hupunguza nidhamu na maadili ya kazi husika.
4 Vyuo au wakuu hawa hafanya jitihada za kuwaondoa maafisa usalama wa vyuo hivyo nakuwapangia majukumu mengine nje ya vyuo au kama watakuwepo basi ni kada ya chini ambao sio tishio kwao kwa namna yeyote.
5 Huchangisha hadi millioni 100 ambazo hutumika kujiimalisha katika nafasi walizopo hii ikiwa ni pamoja na kusambaza migao maeneo yote muhimu ka katika brigedi zao makao makuu hasa kurugenzi ya mafunzo na uhamisho
ILA mawakala hao wamekili kushindwa kuingia chuo cha maafisa TMA kutokana na misimamo kizalendo ya wakuu wanaoka wekwa pale Mbinu hizi ndizo nchi hiyo husika iliitumia kuingia DRC ilikua mkakati wa mda mrefu mwisho wa habali.
Najua watakuja wabishi naomba wafanye tafiti kidogo tu na hili wamelifanya sambamba na kuhujumu ununuzi wa silaha na silaha ktk maghala na magari ya JWTZ katika baadhi ya vikosi.
Hili waliwatumia hutumia watu wenye tamaa ya fedha kufanya haya KAZI KWENU MAKAMANDA KIKULACHO KINGUONI MWAKO wapenda fedha wataliangamiza taifa hilikwa kukosa uzalendo inchi imejaa wasaliti TUAMKE.