JWTZ fungukeni macho mnahujumiwa

JWTZ fungukeni macho mnahujumiwa

Mtoa mada wewe ni mwongo sana na una nia ya kutisha watu bila sababu ya maana,huo ni UZUSHI mkubwa umeleta.
Nimeipata katika nchi jirani iliyokua na vita ya maneno na Tanzania, miaka ya karibuni kumekuwa na hujuma kubwa inafanywa ndani ya JWTZ hasa katika mfumo wa mafunzo kwa kada chini yaani JRN NCOs n SRNCOs katika vyuo vyao.

Swala liko hivi, kitengo cha kijasusi cha nchi hiyo kilituma mawakala nchini kiliwalenga wakuu wa vyuo hivyo vilivyopo TABORA KALUNDE, ZANZIBAR CHUKWANI, DAR ES SALAAM KIMBIJI mawakala walikua na kazi moja tu yakushawishi kulegeza mafunzo ya kijeshi na nidhamuili kuzoletesha ufanisi na utendaji kivita kwa JWTZ na wakuu hao wa vyuo wanafaidika na mgao mkubwa wa fedha toka katika nchi hiyo.

Kinachofanyika ili kutakatisha fedha hiyo wakuu hao hupitisha michango kwa wanafunzi wanaohudhuria kozi ktk vyuo vyao kwa kichwa kimoja huweza kufikia tsh 300000 hadi tsh 500000 kwa mda wa miezi minne ambayo hukaa hapo.

Kumbuka chuo kimoja huchukua wanafunzi kati ya 400 hadi 1000 elfu moja hukusanya zaidi ya tsh 100 millioni mia moja ambazo hazina ukaguzi wowote kwa kisingizio cha ujenzi wa miundo mbinu au huendesha klub za michezo hapo ndio kitendawili kilipo haijulikani kiasi wanakusanya na zinatumikaje sababu huzungukwa na mazingira ya usiri sana.

Pia hili hufanyika kama syndicate mtandao huu upo hadi makao makuu ya jeshi kila mtu hupata kutokana na ushiriki wake, mfano kurugenzi ya mafunzo hushurutishwa kupeleka idadi kubwa ya wanafunzi kuliko miundo mbinu ya vyuo husika lengo ni kupeleka nguvu kubwa kwaajiri ya kupata michango na mgao kwa kila moja ili kufanikisha hayo mambo yafuatayo hufanyika.

1. Chuo hupokea idadi kubwa ya wanafunzi bila uwiano sawa na wakufunzi kwa hili chuo kilichoathirika sana ni Kalunde TC

2 Wakufunzi hasa maofisa waandamizi wanaonekana kua na misimamo ya kukinzana na wakuu hao wa vyuo huamishwa vituoni mara moja na kupelekwa sehemu zingine ili kupunguza makali ya kozi.

3 Hufanya jitahada za makusudi kulegeza mafunzo ili kutoa ushawishi kwa wanafunzi kutoa michango bila malalamiko hili hupunguza nidhamu na maadili ya kazi husika.

4 Vyuo au wakuu hawa hafanya jitihada za kuwaondoa maafisa usalama wa vyuo hivyo nakuwapangia majukumu mengine nje ya vyuo au kama watakuwepo basi ni kada ya chini ambao sio tishio kwao kwa namna yeyote.

5 Huchangisha hadi millioni 100 ambazo hutumika kujiimalisha katika nafasi walizopo hii ikiwa ni pamoja na kusambaza migao maeneo yote muhimu ka katika brigedi zao makao makuu hasa kurugenzi ya mafunzo na uhamisho

ILA mawakala hao wamekili kushindwa kuingia chuo cha maafisa TMA kutokana na misimamo kizalendo ya wakuu wanaoka wekwa pale Mbinu hizi ndizo nchi hiyo husika iliitumia kuingia DRC ilikua mkakati wa mda mrefu mwisho wa habali.

Najua watakuja wabishi naomba wafanye tafiti kidogo tu na hili wamelifanya sambamba na kuhujumu ununuzi wa silaha na silaha ktk maghala na magari ya JWTZ katika baadhi ya vikosi.

Hili waliwatumia hutumia watu wenye tamaa ya fedha kufanya haya KAZI KWENU MAKAMANDA KIKULACHO KINGUONI MWAKO wapenda fedha wataliangamiza taifa hilikwa kukosa uzalendo inchi imejaa wasaliti TUAMKE.
 
Kamanda Chakaza nasema habari hizi sio sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Ni wazi kwa Watanzania wengi kuwa jeshi letu Lina nguvu kuliko majeshi ya nchi washirika(EAC). Taarifa kama hizi si za kufumbia macho. Pia ni kweli kuwa raia wana nafasi katika kutoa taarifa ila tukumbuke kuwa kama kweli Kuna mbinu za kijasusi kukamilisha lengo Lao wao si wapumbavu kwa maana kwamba watajitahidi kwa namba yoyote wafanye kazi Yao kwa usiri na uthabiti. Muhimu vyombo vinavyohusika wafuatilie Hilo na kuchukua hatua stahiki
 
kwani anakosa gani?.au unadhani jamiforum wahusika hawaingi humu.hata hivyo ninawasiwasi na wewe kwa kiswahili chako hicho.

Wacha upuzi kama unakijua kishwahili rudia post yako kisha rekebisha mwenyewe halafu uje ufute kauliyako
 
Si mpaka vita itokee sasa!!isipotoke,na madhara hayataonekana hivyo kufanya zoezi la upigaji pesa kuwa endelevu na lenye kulevya zaidi.


Hili ndio tatizo la sasa,tunaangalia leo na si kesho,unaposema mpaka vita itokee ama isitokee hizo ni fikra za zama za ujima,dunia ya leo vita haipiganwi hovyo,watu wanaandaa long-term plan kwa maslahi ya nchi yao,wanaanzisha chokochoko na nchi nyingine kwa maslahi, wanaangalia weakness ya nchi unayotaka kupigana nayo kwa kudukua taarifa za siri ama kuingiza majasusi kujua una nini ktk ulinzi,suala la ulinzi wa taifa ni nyeti sana na upunguani huu kama wako wa kuingiza wizi/ufisadi ktk masuala ya ulinzi kwa kulipigania tumbo lako na familia yako ni hujuma kwa ulinzi wa taifa.
Tuwe wazalendo.
 
WaTANZANIA tumelala fofofooo nimemaliza kazi yangu kulisaidia taifa langu watu bado wanabisha wakati wenzetu wako katika long term plan sie tuna endelea kudiscus million kumi za mboga haya kwa herini wadau ila wale wanofanyanyia kazi hizi habari najua watakua tayari wameshaona viashiria flani sipendi kwenda mbali naishia hapo
 
sory bro sikuja kubishana huwezi ukapinga tafiti kwa maneno tafiti hupingwa kwa tafiti kwa heri
 
sory bro sikuja kubishana huwezi ukapinga tafiti kwa maneno tafiti hupingwa kwa tafiti kwa heri

nilipoipata hii habari nilijua ni mpya kumbe inajulikana sana tu tatizo kila mtu alikua anaiongelea chinichini hebu tungtuone baada ya miaka 6 nini kitatokea wasipochukua hatua naskia jamaa wanalindwa sana kutokana na uwezo wao mkubwa kiuchumi
 
Hizi taarifa sio ngeni hata kidogo, zipo na zimewahi kuandikwa na gazeti lile lililofungiwa
Walishawahi kukamatwa mawakala kinondoni ishu ikarushwarushwa baadae ikaisha kimyakimya, kwa kifupi tuna wageni wengi mno nchini na wengine wakiwa na mpaka vitambulisho vya taifa
 
Mzani unacheza. . . . . . . .
1. Hiyo michango haina risiti???!!
2. Wakuu wa sehemu husika (chuo) wanamtoa mtu aliye na special task??!!!! Hii hapana. . . . .au anayebaki anakuwa hana madhara unamaanisha nini hapa??!!!
3. Kambi ya watu 400 wakichanga sh 300,000 kila mmoja ni 120M sasa unaposema wanakusanya "hadi" 100M unamaanisha nini??!!!

Taarifa ni taarifa though. . . . . . .

Akili yako ni ngumu kuelewa sana , hizo hesabu ni estimation. We rst umezipeleka huko, we hufai hata kuwa humu jf, akili yako ya kuchanganua mambo ni shida
 
Akili yako ni ngumu kuelewa sana , hizo hesabu ni estimation. We rst umezipeleka huko, we hufai hata kuwa humu jf, akili yako ya kuchanganua mambo ni shida

Sana haswa logic inapogoma. . .. .akili ndogo hujibiwa na majibu makubwa mpaka ione aibu lakini kama akili kubwa inaishia kubwabwaja bila majibu basi tofauti inakosekana!!!
 
Hizi taarifa sio ngeni hata kidogo, zipo na zimewahi kuandikwa na gazeti lile lililofungiwa
Walishawahi kukamatwa mawakala kinondoni ishu ikarushwarushwa baadae ikaisha kimyakimya, kwa kifupi tuna wageni wengi mno nchini na wengine wakiwa na mpaka vitambulisho vya taifa
bora wewe bro
 
Back
Top Bottom