JWTZ kutumwa tena DRC, Rais wa DRC asema kikosi cha Afrika mashariki kinashirikiana na M23 kuimaliza DRC

JWTZ kutumwa tena DRC, Rais wa DRC asema kikosi cha Afrika mashariki kinashirikiana na M23 kuimaliza DRC

Hii vita kuisha kwake ni hadi hayo Madini yaliyopo DRC yaishe.

Unadhani PK anajenga miundombinu ya gharama pale Kigali kwa fedha za Kilimo ambacho nasisi Watanzania tunalima?

Au Utalii upi wa kutuzidi Watanzania
Ni kweli, DRC ndiyo inayokuza uchumi wa Rwanda. Kwahiyo vita haitaisha labda Kagame aangushwe kutoka madarakani. Vinginevyo DRC itaendelea kukuza uchumi wa Rwanda milele
 
Kule DRC kunaonekana kuna hata watu wapo ndani ya drc government na wanashirikiana na waasi.
Juzi hapa general wa kenya kajitoa kule kwenye jeshi la East Africa maana anaona Uganda ambao wapo ndani ya jeshi la east Africa wanatoa siri kwa waasi wa drc.
Vitu ambavyo anajadili pamoja.
 
Miezi kadhaa iliyopita jeshi la east Africa Liliacha kushilikina na rwanda maana waliona rwanda rwanda wanapeleka siri kwa waasi.

Pia general wa kenya amegundua kuwa wanajeshi wa Uganda 1000 waliopelekwa kule baadhi yao wanashilikina na waasi waliokuwa misituni maeneo ya mipaka ya Uganda na rwanda.
 
Rais wa congo yuko mjini Gaborone kwa ziara ya kikazi na leo amesema kikosi cha Afrika mashariki kilichopelekwa nchini mwake hakijafanya lolote la maana na kimeanza kushirikiana na waasi wa M23 na ameziomba nchi za SADC zisaidie.

Mh Rais Samia Suluhu Hassan yupo mjini Windhoek na ameombwa Tanzania kuwa kiongozi wa kikosi kitakacho tumwa DRC hivi karibuni kupambana na waasi wa M23.

Itakumbukwa kuwa kikosi cha SADC kikiongozwa na Tanzania kiliwahi kuwafurahisha waasi wa M23 miaka ya 2010-2014 likishirikiana na wale wa Malawi na South Africa.

My take: kumbe wale wakora wa KDF wako kushirikiana na waasi hii ni hatari sana kwa walinda amani kushirikiana na wauwaji

chanzo RFI

USSR

=======
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amelishtumu jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutofanya vya kutosha kudhibiti utovu wa usalama Mashariki mwa nchi yake.

Tshisekedi ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Botswana na kudai kuwa kikosi hicho kinashirikiana na waasi wa M 23 na huenda kikaondoka nchini mwake kufikia mwisho wa mwezi Juni.
“Kazi ambayo kikosi hiki kilipewa haijatekelezwa kabisa, leo tumeona katika baadhi ya maeneo ushirikiano kati ya kikosi cha jumuiya na waasi wa M23 kinyume na ilivyopangwa kwenye makubaliano.“ alisema rais Felix Tshisekedi

EM Sound - Rais wa DRC Felix Tshisekedi amekosoa utendakazi wa kikosi cha EAC mashariki mwa nchi yake
Kauli yake inakuja siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya SADC nchini Namibia, ambako jumuiya hiyo imesema itatuma vikosi vyake Mashariki mwa DRC.

Matamshi yake pia yanakuja baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kamanda wa kikosi hicho nchini DRC Jenerali Jeff Nyagah katika kile kilichodaiwa ni kutokuwepo kwa maelewano na uongozi wa nchi hiyo ambao pia ulikosoa utendakazi wake.

Meja generali Jeff Nyagah, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya EACRF nchini DRC © EACRF Aidha mkuu huyo wa DRC alisema kuwa muda wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki utakapofika tamati mwishoni mwa mwezi Juni watafanya tathmini kuona iwapo kikosi hicho kitakuwa kimefanya kazi yake na baadae watafanya maamuzi kuona namna watakavyolinda nchi yao ya Kongo.

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC AP - Ben Curtis
Kando na rais Tshisekedi kukosoa jukumu na uwezo wa kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, raia nchini humo pia nao wamekuwa na kauli sawa na kiongozi wakituhumu wanajeshi hao kwa kukosa kutekeleza walivyotarajiwa kufanya.

Licha ya uwepo wa vikosi hivyo katika baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na makundi yenye silaha ikiwemo M23, mashambulio dhidi ya raia yamekuwa yakiendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya DRC.

Waasi wa M23 wanatuhumiwa kwa kuhangaisha usalama wa raia mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa

Japokuwa wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kukosa kuwakabili waasi, baadhi ya raia wameeleza kuwa wamerejea katika makazi yao ya zamani baada ya M23 kuondoka na kupeana sehemu kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nchi za SADC zinajumuisha Afrika Kusini, Angola, Tanzania, Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na DRC.

Mkuu ndani ya jeshi la africa mashariki kuna kenya ambaye ni kiongozi, Tanzania ,Rwanda, Uganda na Burundi, na South sudan.

Shida ilianza kwa baada jeshi la east Africa kuwaingiza Magenerali wa rwanda kwenye Vikas vya kujadili usalama wa congo.
Ikanonekana wanatoa siri kwemda Kigali na makundi ya uasi drc.
Baadae wakatoa barua east Africa kuwatoa rwanda wakafanikiwa.

Baada ya kama mwezi Uganda wakapeleka wanajeshi 1000 kulinda drc.
Ila uchunguzi ukaonekana baadhi ya viongozi wa Uganda wanapeleka majadiliano kwa waasi.
Na Generali wa kenya kasema kuwa itakuwa ngumu maana inaonekana wale wanajeshi 1000 wa Uganda baadhi yao wanafanya kazi na waasi kama m23 ambao sasahivi wapo kwenye vijiji vya congo ila mpakani mwa Uganda na rwanda.
Na kumbuka still Burundi pia kuna watusti.
Ndo maana jeshi la Africa mashiriki linaonekana sio kitu.
●KUNA USALITI NDANI YA JESHI KULE LA AFRICA MASHARIKI SIDHANI KAMA WANGEFANIKIWA KWENYE OPERATION YAO HIO●
 
Kama ningekuwa Rais wa TANZANIA ningepelekea Full kikosi hapo Mashariki ya DRC yaani ni Full Vita, lengo ni kulinda Maslahi mapana ya nchi yetu hasa Kiuchumi.

DRC imekuwa nchi muhimu sana kwa uchumi wetu, hapa ndipo unapomuona USA katili, yy ukiisumbua nchi aliyo na maslahi nae atadeal na ww kwa kila hatua.

RAIS SAMIA, amua kupeleka kikosi kamili hapo DRC tutengeneze wigo wetu wa uchumi, hii ndio njia ya kujiwekea hali salama na uchumi imara, tulinde masoko yetu.

Ningekuwa Rais wa TZ naamini muda huu KAGAME sio Rais wa Rwanda, lazima ningepandikiza Mtz kama ilivyokuwa BURUNDI, UGANDA, DRC wakati wa KABILA.

Ukanda huu msumbufu ni KAGAME, na ningeshamuondoa madarakani, iwe kwa Demokrasia au kupinduliwa.
 
Huyo jenerali ndiye aliyekuwa anashirikiana na m23, kaona maji yamemfika shingoni kajiuzuru.
Askari wa chini yake kumwacha akijiuzulu bila kumshughukia kijeshi hawajakitendea haki jeshi la Kenya alitakiwa kurudi Kenya akiwa kwenye jeneza Askari walio chini yake wangemalizana naye

Kwa nini? Yeye kama kamanda kama msaliti anasababisha Askari wadogo kupigwa Risasi na kuuawa na M23 yeye akiwa tu anakula nao pizza na chips kuku

Askari wadogo walitakiwa wamuue arudi maiti Kenya

Sababu aweza toa maelekezo mabovu kwa kujikomba kwa M23 yakasababisha Askari wadogo kufa dawa ilitakiwa kumuuua akiwa kongo maiti wampelekee Ruto wanwambie M23.wamemuua vitani kwa ambush

Kamanda vitani anatakiwa kutokuwa muoga wala kuungana na adui ina cost Askari wadogo waweza uawa kama kuku vitani

Askari wadogo wa jeshi la Kenya walioko kongo hawajalitendea haki jeshi lao Kenya huyo Generali alitakiwa arudi Kenya akiwa kwenye jeneza
 
Back
Top Bottom