JWTZ kutumwa tena DRC, Rais wa DRC asema kikosi cha Afrika mashariki kinashirikiana na M23 kuimaliza DRC

Mkuu watu wanabeza tu, ila JWTZ sio mchezo.
 

Sijaona mahali popote JWTZ as you have highlighted, zimeorozeshwa nchi, hakuna mahali popote wamewema Tanzania itaongoza...
 
Hii vita kuisha kwake ni hadi hayo Madini yaliyopo DRC yaishe.

Unadhani PK anajenga miundombinu ya gharama pale Kigali kwa fedha za Kilimo ambacho nasisi Watanzania tunalima?

Au Utalii upi wa kutuzidi Watanzania
Rwanda ni ka mkoa ka Tz, analima nini yule?
 
Waachane waende vijana wetu kwenye mission Ni miezi mitatu tu Hali itatulia kbsa
 
Hao M23 kiboko Yao n JWTZ dk sifuri wanawaludisha Rwanda.
Hapana. Sio kuwarudisha Rwanda - JWTZ hawanaga taimu kufanya biashara hiyo bali ni kuwasambaratisha na kuwateketeza kabisa. Kwa Watakaobahatika kusalia wakiwa hai watarudi wenyewe Rwanda fasta.
 
Wakishafika pale wakipewa channel ya kupiga hela wanaachana na kazi iliyowaleta wanaungana na waasi.
Mfano Jeshi la Kenya lilivyoenda na Presha kubwa Watu wakapata matumaini mapya Baada ya muda mfupi walivyoonyeshwa na WTz Namna ya kupiga hela hatujasikia tena Lile Jeshi la Kenya
Matokea yake tunasikia wananchi wakilalamika kutaka waondoke
 
Tulisema humu, KDF ni jeshi la ovyo! Sasa mngeona siku wanaenda DRC hiyo mikwara! Hakuna vita wanaweza wale!
 
Waache visingizio, ni military intelligence failure! Walipaswa kujua hilo before! Au kutengeneza mfumo wa kunyooshana siri ikivuja. Hata ndani ya nchi kuna kuhujumiana ila adhabu ya msaliti inafahamika!

Kenya wamepewa jukumu la kuongoza mapambano alafu wameshindwa ku control operations. Hizi zinataka umafia tu, mwendo wa kufyekana kulinda heshima
 
Ndiyo maana juzi hapa alimtembelea bimkubwa, ukute alishajua kinachoendelea, akawahi kubargain.
AMBACHO NIMEKUWA NAJIULIZA BILA MAJIBU, NI KWA NINI JWTZ HAWAKUJUMUISHWA KWENYE KIKOSI CHA AFRIKA MASHARIKI ILHALI WANAIJUA HISTORIA YAKE?
Tayari tuna maslahi ya kijeshi na SADC, hawa wahuni vikao vya wachawi havidumu!
 
Commando unit ya jwtz ipo drc tayari hivi ninavyoandika.
mkono mtupu haulambwi ....weka ushahidi hapa...wa sijui comando Unit JWTZ.......wapo DRC....[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Hivyo vita vya DRC ni utoto mtupu.

Waasi wakizidiwa wanaomba mazungumzo na serikali wanakubaliana kusitisha vita na masharti ya wapiganaji wao kuandikishwa jeshini.

M23 ya Colonel Makenga ilikuwa tayari imejifia miaka 10 iliyopita.

JWTZ wasipelekwe huko.
 
Ndiyo maana juzi hapa alimtembelea bimkubwa, ukute alishajua kinachoendelea, akawahi kubargain.
AMBACHO NIMEKUWA NAJIULIZA BILA MAJIBU, NI KWA NINI JWTZ HAWAKUJUMUISHWA KWENYE KIKOSI CHA AFRIKA MASHARIKI ILHALI WANAIJUA HISTORIA YAKE?
Walikataa (military intelligence ilikuwa makini saana pongezi kwao)
 
Wacomgoman wajifunze kuacha kuendekeza mambo ya starehe na wanawake - muziki 24X7 - likitokea la kutokea ndio wanakwenda kuomba msaada wa kijeshi kutoka kwa nchi jirani, hawana hata mpango wa kuwapatia mafunzo ya kijeshi ya nguvu na nidhamu ya hali ya juu vijana wao - jeshi bila midhani na uzalendo ni sawa sawa na hakuna - ndio maana wanajeshi wake wasikia tu mlio wa mzinga au triple A's- wanatimua mbio mpaka wanapotezana.

Ndio maana siku za nyuma nilimshauri Tshekedi amuombe Putin azungumze na CEO wa Wagner Group ili awapatie wanajeshi wa Congo DRC mafunzo ya kijeshi ya hali ya juu na nidhamu juu.

Sio kila saa kuwapeleka wanajeshi wetu kwenda kuwasaidia wanajeshi ambao hawana nidhamu au kujielewa wamebweteka kabisa - ya nini kuendelea kuhatarisha maisha ya vijana wetu hii mpaka lini

Tsishekedi anapashwa kuelezwa na viongozi wa SADC na EA ukweli kwamba mwenye jukumu la kuhakakisha ulizi wa taifa lake ni yeye mwenyewe - msaada wa kijeshi uje tu inapo bidi sio kila tukio.
 
Ndiyo maana juzi hapa alimtembelea bimkubwa, ukute alishajua kinachoendelea, akawahi kubargain.
AMBACHO NIMEKUWA NAJIULIZA BILA MAJIBU, NI KWA NINI JWTZ HAWAKUJUMUISHWA KWENYE KIKOSI CHA AFRIKA MASHARIKI ILHALI WANAIJUA HISTORIA YAKE?
Ni Kwa sababu TZ wakijua Kuna usnitch ndani ya kikosi Cha EAC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…