JWTZ kuwatesa raia wanaovaa nguo za Jeshi ni ukatili

JWTZ kuwatesa raia wanaovaa nguo za Jeshi ni ukatili

Hivi kwa huu unyama unaotendeka hapa chini hili linafaa liitwe jeshi la Wananchi wa Tanzania au jeshi la Maharamia dhidi ya wananchi wa Tanzania?

CDF haya ndio mafunzo mnaowapa vijana wenu dhidi yetu Watanzania wenzao?

Ni sheria gani ya nchi na hapo jeshini inaruhusu huu upuuzi unaofanywa na hawa makamanda dhidi ya huyu mtu ?

Hivi hawa askari wanatengeza chuki gani kati ya jeshi na wananchi?

Naomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa hawa makamanda wote waliofanya huu upuuzi.

Wangewakamata wanaoingiza na kuuza hizo nguo
 
Zamani ilikuwa ukivaa kitambaa chochote che kufanana na bendera ya taifa upo matatani, watu wakahamia kuvaa bendera za US, UK, Zambia, serikali ikaona mmmh!!! Ikabidi polepole inyamaze
 
Nilijua ni wanajeshi wachache wasio jielewa wanafanya mambo kama hayo nilijiprove wrong nilipoona kiongozi jeshini anabariki suala kama hilo kwa kutoa siku kadhaa na baada ya hizo siku watakaobainika kukiona

Kauli ile ni sawa kabisa na kubariki vitendo vya kunyanyasa raia namna hiyo wajitafakari sana hawa jamaa matendo kama hayo ni usela wa kizamani sana watu tulishahama level hizo
ni hivi wanatafuta nguo za kuvaa... salikuja golini wamewakuta madogo wamechukua kila kilichokua na maaua mfano wa batic.. beba masweta na makot... mabegi nk.... iko siku tutaficha waasi mitaani ili wawashikishe adabu ndio watajua wayafanyayo wanatufunza uzalendo au usaliti.
 
20230917_124639.jpg
20230917_124632.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila jeshi waache majukumu yao ya msingi na waanze kutafuta sare zao, jeshi la police nao wanakuja mtaani kutafuta sare zao, magereza nao wanakuja, zimamoto nao wanakuja, uhamiaji nao wanakuja, na mgambo nao wanakuja hadi suma jkt nao waje itakuaje sasa maana kigezo cha kufanyia utapeli ni cha kipumbavu
 
Halafu ajabu tabia hii ya hivyo ipo tanzania pekee.
 
Form four failure wana jipya gani humo majeshini? Wanachokijua ndio kama hiki kinachotendeka humo videoni
 
Hivi bado hili katazo lipo active....mana leo nimetinga na pensi ya mabaka mabaka
 
Back
Top Bottom