JWTZ kuwatesa raia wanaovaa nguo za Jeshi ni ukatili

Wangewakamata wanaoingiza na kuuza hizo nguo
 
Zamani ilikuwa ukivaa kitambaa chochote che kufanana na bendera ya taifa upo matatani, watu wakahamia kuvaa bendera za US, UK, Zambia, serikali ikaona mmmh!!! Ikabidi polepole inyamaze
 
ni hivi wanatafuta nguo za kuvaa... salikuja golini wamewakuta madogo wamechukua kila kilichokua na maaua mfano wa batic.. beba masweta na makot... mabegi nk.... iko siku tutaficha waasi mitaani ili wawashikishe adabu ndio watajua wayafanyayo wanatufunza uzalendo au usaliti.
 
Kila jeshi waache majukumu yao ya msingi na waanze kutafuta sare zao, jeshi la police nao wanakuja mtaani kutafuta sare zao, magereza nao wanakuja, zimamoto nao wanakuja, uhamiaji nao wanakuja, na mgambo nao wanakuja hadi suma jkt nao waje itakuaje sasa maana kigezo cha kufanyia utapeli ni cha kipumbavu
 
Halafu ajabu tabia hii ya hivyo ipo tanzania pekee.
 
Form four failure wana jipya gani humo majeshini? Wanachokijua ndio kama hiki kinachotendeka humo videoni
 
Hivi bado hili katazo lipo active....mana leo nimetinga na pensi ya mabaka mabaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…