JWTZ mpaka leo imeshindwa kuajiri wasomi wenye vipaji halisi, sababu hizi hapa...

mada ilikua nzuri ila mmeiaribu kwa mashindano yasiyona maana.sijui lini watanzania mtatumia akili
 


jeshi waanajiri watu....makini kutoko vyuo makini ...kwa mfano kama mfano vyuo kama
1.udsm
2.mzumbe
3.d.i.t
4.sua
ni vyuo ambavyoo hutoa wasomi bora....ndo maana jeshi huamini vijana toka huku sasa kama wewe ulisoma chuo cha kizushi karisit mitihani ya form 4 na 6...ili uende ukasome vyuo hivi vyenye ubora utapata tuu kazi tuu jeshini
 
Wanaojua mambo ya jeshi na wajue na wasiojua mtafute nafasi muingie kama mna qualifications zinazohitajika maana hata kwa kosoma mitandaoni sidhani kama mtajua ile reality ya ukiwa mafunzoni jeshini. Mtoa mada nadhani atakuwa alishindwa pale TMA au hakupita kwenye interview pale KUNDUCHI. Huko kinachoangaliwa ni OBEDIENCE TO LAW, RULES AND AUTHORITY ONLY.
Sasa kama wewe ulienda na degree au masters yako then ukawa unajifanya wewe ni mjuaji kwa wale maaskari, hiyo imekula kwako kaka. Jambo la kwanza ni lazima utolewe URAIA kwa mambo ambayo unaweza sema wanakudhalilisha na wengi hapa ndipo wanapotorokaga au kuonesha jeuri zao ambazo zinawaletea shida na mwisho kufukuzwa kama si kuishi maisha ya taabu na wakufunzi. Yangu hayo na Heri ya mwaka mpya
 
Sio siasa fikiri kwa kutumia akili kichwa na sio ma...
Huwa makalio yangu yanafikiri kwa kina zaidi kuliko kichwa chako, na wewe unajua hilo ndio maana uka refer!
sasa nikija tumia kuchwa hutaona ndani!
 
Maisha si lazima uwe mwajiriwa wa JWTZ tu, kama unajiona una CV ya kutisha tafuta Taasisi zingine ambazo zitakunyenyekea pamoja na unanga wako, kiburi chako na utovu wako wa nidhamu, kisha na mavyeti vya kununua toka ulikotoka !!
Kwa taratibu za kkawaida tu, ukishindwa kumheshimu mdogo, je huyo wa juu yako utamheshimu kweli kwa dhati au ndio unafiki !!
Jiunge na siasa uingie Bungeni, ili umalizapo tu kiapo uanze kuwahadaa Wa-tz kwa Mikataba ya kuliuza Taifa !!
 

(Nimesimama mguu sawa na kupiga saluti) Afande umeua!
 

For me, this is the best comment

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ratio nota Masada amekurupuka,
anaongea vitu ambavyo Hana detail navyo,kutengeneza ofisa aw jeshi sio kazi raisi Kama unavyodhani, ukija module degree Chako unakiacha Getini, pale wote ni cadet
 
For me, this is the best comment

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Good comments, lakini msiwalaumu wakufunzi wa JWTZ kwani mfumo mzima wa vyuo vyetu ni wa kivita kati ya mwalimu na mwanafunzi, mwalimu anajisikia raha au bingwa kufelisha kundi kubwa la wanafunzi na anapata support kubwa na maelezo ni kuwa wanafunzi ni vilaza. Inakuaje mwanafunzi tangu darasa la kwanza anafanya vizuri mpaka form six, halafu chuo anakua kilaza???

Inawezekana wanafunzi ni tatizo lakini nafikiri kunahaja yakuangalia kwa undani hili suala. Mwalimu akimchukia mwanafunzi basi atafeli, why? kwa maslahi ya nani??? Taifa kweli litaendelea hivi!!!! Nionavyo mimi wengi wanaofanya hii kazi ya uwalimu/ukufunzi wamelazimishwa aidha na mazingira au na mfumo, kwani binadamu wakawaida atapenda kusifiwa au kujisifu kwa matokeo ya kazi nzuri aliyoifanya.

Kwakweli itokee mwanafunzi amefeli kwakuwa hana uwezo. Implication ya mfumo huu wa wakunfunzi kuwafelisha au kujisikia hodari kwa kufelisha unawafanya wanafunzi vyuoni kote iwe jeshini au uraiani wasijifunze kwani wakati wote wanawaza kupambana na audui yake mwalimu. Therefore, cheating, hongo na rushwa vinakidhiri kwakuwa kipimo nikufaulu au kufeli kwenye makaratasi. Tubadilikeni jamani, nidhamu isijengwe kwa vitisho, ije yenyewe automatically.
 
Siku zingine ukileta mada hata kama ni ya majungu jitahidi kuukaribia ukweli kuliko huu ----- uliouandika,kuuliza sii ujinga penda kujifunza inaonekana mtoa hoja huna ufahamu wa uliyoyaandika .
 
Nimeupenda huu uzi, unafundisha.unaburudisha na unaghabisha!
 

Mkuu Mwita Maranya nikuhakikishie tu kuwa duniani kote hakuna kozi za wasomi na wasiosoma. Mafunzo ya kijeshi yako standard no matter what. Ukiwa katika uwanja wa medani bahati mbaya masters yako haitokusaidia kama hujaiva kimbinu. Ndo maana hata corporal ambaye ni competent anaweza kuitikisa nchi. (Nadhani unamkumbuka Iddi Amini). Tena ukihudhuria vyuo vya nje huwezi amini, ni balaa zaidi. Wanakuambia kwamba technology fails, that is why we don't use it in training. Kule kila kitu ni manual tofauti uongo wanaopeana watu. Technology utafundishwa kwenye unit yako sio chuoni. Tatizo wabongo wanafikiri digitali ina affect basic soldiering, no way.Wale wanaotamani kuonda maisha wavumilie kupitia katika kikaango kwanza, ndo wakakae maofisini na bachelors na masters za mambo ya utawala.

Na pale mnaposema vipaji maalum I can't understand what you are driving at? Jeshini vipaji maalum hupelekwa Commando, PT na sehemu nyingine zinazohitaji outstanding performance. Sasa hivi vipaji maalum sijajua ni nini. Nadhani mnamfahamu Balati. He was the greatet leader of all time katika commando, na huyo ni mmoja tu. Alipata bachelor na masters akiwa karibu kabisa na kustaafu. Kumbe basi jeshini kuna askari wengi sana wenye military knowledge ya hali ya juu kuliko most of graduates. Siwapondi hawa, isipokuwa tu kuna notion fulani imejengeka kwamba wasomi wanachukiwa jeshini, lakini ukweli ni kwamba wanaojiita wasomi wengi wao hawapendi kupitia rigorous training. Wanataka watambuliwe usomi wao wakati wa mafunzo kwamba mimi ni daktari, mhasibu, mchimi, n.k. Wakati wa training haya mambo hayana maana yoyote, na ndipo competent corporal ukimtishia elimu yako atakuwa willing kukudhihirishia kuwa katika kile ulichofuata pale, yeye ni zaidi yako. Guys, it is the matter of self discipline, that's all it takes. Otherwise mtabaki ku-lament kila siku kama hamtaki kutambua kuwa military knowledge is a profession in itself.

Daktari akifuzu mafunzo atatakiwa kutibu majeruhi mstari wa mbele, bunduki begani.
Mhasibu atatumia bachelor yake kulipa mishahara mstari wa mbele (vitani mishahara hulipwa kama kawaida).
Logistician atafanya kazi kupeleka logistics frontline (tena hawa huwindwa sana vitani).
N.k. Sasa usipokuwa trained utaperform vipi majukumu hayo? Tusilewe na kazi za jeshi wakati wa amani, kikinuka watu huvua kombati na kujificha, don't be one of them! Just do your part and everything should be fine.

MILITARY TEACHES YOU HOW NOT TO DIE!!!!!!!!!!


 
Asante Nyenyere,

Kama maandishi hayatoshi, picha imefunga kazi! Tatizo la wasomi vijana la kujiona bora kuliko wengine haliko jeshini tu! Hata uraiani ni hivyo! Maofisini ndo kabisa, na bahati mbaya huko wanadekezwa. Pelekeni hoja Serikalini, vijana wote wasomi waende jeshi miezi 4 kabla ya kupata ajira si serikalini tu bali hata Makampuni binafsi.
 

Mkuu unajua kuna watu wnapotoshana sana humu JF. Mwaka 2005 ilivuja video inayoonyesha royal marines (COmmando) wa uingereza wakifanya mazoezi ya magumi uchi wa mnyama. Magazeti na mitandao ilishutumu sana kitendo hicho cha "kidhalilishaji." Hasa kwenye ile sehemu ambapo kuruta alikula mkono hadi akazirai. Sasa "wasomi" wakaanza kuhoji mantiki ya kufanya vitendo kama vile.


Kuna jamaa mmoja katika kutoa maoni yake aliandika sentensi moja tu, lakini yenye majibu yoote:

"Gee, army guys being army guys... go figure. "
Na ujumbe huu uwafikie wale woooooote wanaonung'unikia mafunzo ya jeshi. Siri kubwa ya mwanajeshi ni kuwa Mentally tough. Na hii inapimwa kwa kuwa exposed kwenye mambo ambayo logic ya kawaida itayaita upuuzi. Na mambo haya yataendelea kuwa ni upuuzi mtupu kwa wasomi wetu mpaka pale watakapojikuta ni mateka mikononi mwa adui. Hapo watakumbuka kumbe yale yalikuwa mafunzo muhimu mno kwa kukujenga kisaikolojia. Huko watakutana na mambo ambayo kama wasingepitia hivi vipimo vidogo vidogo vya kuambiwa wenye digrii wadeki vyoo, wasingeweza kusurvive hata dakika tano tu. Wangemwaga yooote.

When the going gets tough, the tough get going. What about the weak? Hawa wanakuwa eliminated na ndo hawa hawa wanakimbilia JF kutafuta huruma. No way!
 
Nina master ya Sheria ya LLB natarajia kujiunga na JWTZ mwakani. Inaonekana huyu mdau alisoma chuo Kikuu cha kata cha UDOM na alipata degree ya sheria ya Pichu. Amedhalilisha professional ya Law
 
Wakuu, wengine mnajadili vizuri na baadhi mnapotosha maada. La msingi tuangalie kwanini kama fedha na rasili mali kibao mnazopewa na serikali kuendeshea jeshi letu mpaka leo hatuioni chochote. Mfano Irani wanafanya mambo makubwa sana na kila mtu humu jf analijua. Lkn hili letu halina hata kimoja cha mfano vyote nyie mnababaisha tu. Angalia pale Lugalo hakuna hata research moja inayofanyika kwanini kama kweli mmna weza kufundisha kwa weledi? Msibishe kwa kasumba ambazo hazina maana jitathimini je hiki ninachokisema sio kweli. Sisi tunawajua udhaifu wenu. mnadfai kulifanyia jeshi reform wakati hamjui sababu ya nyinyi kuwa kama mlivyo. JWTZ hamuwezi bila kufanya research mkabadilika kama mnavyotaka. Mawazo mapya lazima muyakubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…